• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Newala Town Council
Newala Town Council

Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano ya Umma
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi, Maliasili na Mipango Miji
      • Kazi
      • Usafi na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Video
    • Maktaba ya picha

Mhe. Byakanwa awataka wananchi wa Newala kushiriki kimamilifu uchaguzi serikali za mitaa 2019

Posted on: September 24th, 2019

Mkuu wa Mkoa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa, amewataka wananchi mkoani humo kujitokeza kushiriki uchanguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019, kwa kujiandikisha, kupiga kura pamoja na kuwania nafasi ya mwenyekiti wa kijiji, mtaa au kitongoji.

Ameyasema hayo mwishoni mwa juma lililopita akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilayani Newala ya kuongea wa watumishi wa umma, madiwadni, wakandarasi na wafanyabiashara kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na kampeni aliyoianzisha ya Shule ni Choo.

Mhe. Byakanwa amesema uchaguzi huo ni wa kitaifa na litaanza zoezi la kujiandisha kwenye daftari la mpiga kura, kwa kila mtanzania mwenye akili timamu na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea kujiandikisha kwenye kitogoji chake, kuanzia tarehe 08/10/2019 hadi 14/10/2019, na kufuatia na uchaguzi wenyewe utaofanyika tarehe 24/11/2019.

Mkuu wa mkoa amewataka madiwani, maafisa watendaji kufanya mikutano na wananchi kuwaelimisha juu ya umuhimu wa uchaguzi huo kwa na kuwahamasisha watu wenye umri wa miaka 21 na kuendelea wenye sifa za kuwa viongozi bora wajitokeza kuwania nafasi hizo katika maeneo yao bila kubagua jinsi zao.

Sambamba na hilo Mkuu wa mkoa pia ameendelea kuhamasisha kampeni yake ya shule ni Choo kwa wananchi, viongozi, taasisi binafsi na za umma kwa ajili ya kutatua changamoto ya upungufu vyoo vya waalimu na wanafunzi kwenye shule zenye mapungufu baada ya kubaini upungufu huo mashuleni.

Aidha amesema wakurugenzi wanalo jukumu la kuhakikisha wanabuni mbinu na mipango mingine ya kufanikisha mpango huo na kama wananchi wataamua kuwekeza kwenye mambo madogo madogo, upo uwezekana wa nchi kupiga hatua kubwa ya maendeleo waliyosababishwa na wananchi wenyewe.

Katika kikao chake na wakurugenzi, watumishi wa serikali, wakuu wa taasisi na madiwani kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya Newala, ilifanyika harambee ya kampeni hiyo ambapo kwa pamoja jumla ya mifuko ya saruji 679 iliahidiwa na fedha Tsh.8,250,000/= ziliahidiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Newala, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Newala Mhe. Chitwanga Rashid Ndembo, amesema watayazingatia maagizo ya kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi hasa wa vijijini pamoja na kuunga mkono kapeni ya Shule ni Choo kwa vitendo.

Kampeni ya Shule ni Choo mkoani Mtwara imeanzishwa na Mkuu wa mkoa baada ya kubaini uhaba vyoo na vyoo visivyo salama na rafiki kwa matumizi ya waalimu na wanafunzi wawapo shuleni, na kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12/10/2019 na Rais Mstahafu awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akimbatana na waziri wa afya na waziri wa elimu

Kauli mbiu yake ni “Changia Sasa ili Uweze Kumsitiri Mwalimu na Mwanafunzi Wakiwa Mazingira ya Shule.” mtu aneweza kuchangia fedha, malighafi watakayowezesha kufanikisha ujenzi wa vyoo hivyo au kujenga choo chenyewe.



Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA (PSLE) 2019 October 15, 2019
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili nafasi ya Katibu Mahsusi November 11, 2019
  • Mjina ya watumishi wa umma walioteuliwa kuandikisha Wapiga Kura October 03, 2019
  • VIWANJA VIWANJA November 18, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mwenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa waapishwa leo tayari kuanza majukumu yao

    November 27, 2019
  • Idara ya kilimo yatoa elimu kwa mawakala wa uuzaji mbolea ya kukuzia (UREA) kuhusu bei elekezi

    October 24, 2019
  • Kamati ya Lishe Newala Mji, yasisitiza wafanyabiashara kuacha kusambaza chunvi isiyo na madini joto

    October 23, 2019
  • Halmashauri ya Mji Newala kinara kwa kufaulisha darasa la 7 mwaka 2019 mkoani Mtwara,

    October 22, 2019
  • Tazama zote

Video

Mapokezi ya mwenge wa uhuru Halmashauri ya Mji Newala
Video nyingine

Kurasa za Haraka

  • Sanitation day
  • Tender
  • Uhuru torch

Kurasa Mashuhuri

  • Higher Education Students' Loans Board
  • National Examinations Council of Tanzania
  • Tanzania National Electoral Commission
  • PSPF Pension Fund
  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration and Local Government

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Newala-Mtwara

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 39

    Simu: (+255) 023 2410673

    Mobile: PS (0684439199)

    Barua pepe: info@newalatc.go.tz

Other Contacts

   

    • Disclaimer
    • Sera ya Faragha
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya eneo la tukio
    • Huduma

Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa