Saturday 18th, January 2025
@Newala
Halmashauri ya Mji Newala imepokea simu 61 kutoka shirika la ufadhili wa masuala ya afya la nchini Ujerumani GIZ kwa ajili ya mradi wa kuboresha taarifa za uandikishaji majina ya wanachma wa Mfuko wa afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa.
Mkabidhiano ya msaada huo yamefanyika siku ya Alhamis Mei 9, 2019, baina ya mwakilishi wa GIZ mkoani Mtwara Bi. Mariam Omari na Mkurugenzi wa halmashauri akiwa sambamba na waratibu wa idara ya afya wa hospitali ya wilaya inayosimamiwa na halamashauri hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Newala ndg. Andrew Mgaya (kushoto) akipokea simu za masaada wa GIZ ofisini kwa kwake mjini Newala kutoka kwa mwakilishi wa GIZ Bi. Mariam Omari.
Mwakilishi wa GIZ Bi. Mariam Omari (kulia) akikabidhi viambata vya manunuzi kwa Afisa manunuzi wa halmashauri ya mji Newala bwana Sumwike Kajela.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Newala ndg. Andrew Mgaya (kushoto) akikabidhi simu kaimu Mganga mkuu wa halmashari ya mji Newala Dkt. Emanuel Athanas.
Kaimu Mganga mkuu wa halmashari ya mji Newala Dkt. Emanuel Athanas (kulia) akikabidhi simu kwa mratibu wa mfuko wa afya ya jamii.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa