Wakulima Nchini wametakiwa kutambua wanao mchango mkubwa wa kuchangia pato la Taifa kupitia shughuli zao za kilimo hivyo ni huhimu kushikamana na kuungana katika kufanikisha malengo ya Taifa na kuinua uchumi wao.
Hayo yameelezwa siku ya Jumamosi June 13, 2020 na Afisa Kilimo wa halmashauri ya mji Newala Calistus Komba katika kikao cha pamoja cha wakulima wa skimu za umwagiliaji Chikwedu Chipamanda Newala na Lipalwe wilayani Tandahimba cha kujadili ushirikiano wa kufanyakazi pamoja katika skimu hizo zilizo eneo moja.
Komba amewapongeza wakulima hao kwa hatua hiyo nakuitaja kuwa ni hatua ya mafanikio na ni vema waelewe mchango wa wakulima ni mkubwa kwa taifa na ndio maana serikali iliamua kufanya uwekezaji wa kujenga miundombinu ya umwagiliaji ili kuwawezesha wakulima kufanya shughuli zao pasipo kutegemea msimu wa masika.
Akizungumza Katibu wa muda wa muungano huo ambaye pia ni Katibu wa skimu ya Chikwedu Chipamanda Bw. Juma Mnoji amesema muungano huo umelenga kuyanusuru maeneo ambayo hayatumiki na kwa kuwa wapo watu amabao hawana maeneo na wapo tayari kufanya shughuli za kilimo nao waweze kupatiwa maeneo ili kila mmoja naufaike tofauti na ilivyo hivi sasa watu wanayashikilia maeneo ambayo hawayatumii.
Naye Mwenyekiti wa kikao hicho Bw. Mnyunda Halfani ameiomba serikali kuwapa ushirikiano ili malengo yafikiwe kwa kuwa wapo wakilima wanaokiuka makubaliano kwa makusudi huku Afisa Mtendaji wa kijiji cha Lipalwe B, Bw. Juma Mnyenje akiwata wafugaji wa ng’ombe kuzuia mifugo yao isiaribu barabara zilizopo na mazao ya wakulima ili kuepusha migororo isiyo ya lazima ukizingatia kazi ya kilimo ni ngumu na inatumia muda mwingi katika maandalizi.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho Bw. Hafidhi Matola, Juma Omari, Bi. Sofia Kahango na Zena Kaisi Baraka wamesema wapo tayari kushirikiana kwa nguvu kufanyakazi na kuilinda miundo mbinu kwa kuwa hata sasa wanapata faida kubwa huku wakiwataka wanawake kutokua nyuma katika shughuli hiyo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa