Vikundi vya vijana wajasiriamali vilivyopewa mkopo na halmashauri ya mji Newala vimeonywa juu ya kutorejesha mikopo waliyopewa kwa kuwa mikopo hiyo ni lazima irejeshwe na inufaishe wengine kama lengo kusudiwa la serikali lilivyo.
Hayo yameelezwa mkuu wa idara ya maendeleo ya jamaii Bi. Frola Barakana wakati wa semina elekezi ya namna ya kutumia na kurejesha fedha hizo iliyofanyika leo Ijumaa 21/02/2020 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Barakana amesema vikundi vingi vya vijana nimekua na changamoto ya kutoendeleza miradi na badala yake wanagawana fedha na kukimbia naeneo wanayoishi kwa lengo la kutorejesha mikopo hiyo lakini kwa utaratibu wa sasa hatua kali zitaendeleo kuchukuliwa na hakuna atakayeza kukimbia.
Aidha amefafanua kuwa serikali kupitia halmashauri inatoa mikopo hiyo bila riba kwa vikundi vya wanawake, walemavu na vijana na jumla ya vikundi 27 vyenye wanachama 192 kwa awamu hii wamekopeshwa jumla ya shilingi miliioni 67.5.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa Wajasiriamali halmashauri ya mji Newala Bw. Ahmed Naheka amevitaka vikundi hivyo kujiunga na umoja huo ili kupata fursa mbalimbali za kibiashara kama kushiriki maonesho mbalimbali ya bidhaa, kupata masoko, elimu ya biashara na namna ya kuongeza thamani ya bidhaa zao.
Bi. Marium Mneno mwakilishi wa walemavu na Bw. Shazil Yahaya Hamisi mwakilishi wa vijana wameishukuru serikali na idara ya maendeleo ya jamii kwa kuanza kuwapa uelewa na ushauri juu ya usimamizi wa miradi na kuahidi kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iwanufaishe wengine.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa