Afisa Mazingira wa halmashauri ya mji Newala Bw. Hyasinty Msanga amewataka wajasiriamali wadogo, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, kuacha kuitumia mifuko ya plastiki kama serikali ilivyoagiza ili kuepuka faini zisizo na lazima.
Rai hiyo ameitoa leo Jumanne Agosti 27, 2019 akiwa ofisini kwake, mara baada ya zoezi la kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa soko kuu Newala, kuhusu matumizi sahihi ya vifungashio vya bidhaa kwa wateja wao.
Msanga amesema hatua hiyo imekuja baada ya uwepo wa uzalishaji na matumizi ya mifuko laini ya plastiki ambayo haijakidhi viwango hivyo baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), chini ya Wiraza ya Ofisi ya makamo wa Rais Muungano na mazingira, Agosti 16 mwaka huu lilitoa wiki mbili ili watu wasitishe matumizi na uzalishaji wake.
Hata hivyo Msanga amesema kumekua na tabia ya wananchi kupuuza maagizo mbalimbali yanayotolewa na serikali, hivyo amewasihi kuachana na mifuko hiyo ili kuepuka usumbufu wa kulipa tozo, kwani faini zake zinaanzia shilingi elfu 30 hadi milioni 50 au kifungo cha kuanzia siku 7 hadi miezi 3 na halmashauri kupitia ofisi yake itasimamia zoezi hilo kama baraza lilivyoelekeza.
“Kuna mifuko ya plastiki ambayo imetengezwa siku hizi ni myeupe alafu imekua myepesi, kiasi kwamba inauwezo wa kuchukua kilo moja, wananchi wengi wamekua wakiitumia mifuko hii ya plastiki kuifadhia nyama, vituu n.k, lakini baada ya kufanya utafiti ikaonekana mifuko hii haijakidhi viwango hivyo baraza likatoa notisi ya kusitisha kuzalishaji na uuzaji”, amefafanua Msanga.
Aidha amesema, NEMC imewataka watu kuacha kuzalisha, kuifadhi, kusambaza, kumiliki na kutumia mifuko hiyo, badala yake watumie mifuko mbadala iliyoelekezwa na mpaka jana Agosti 26, 2019 jumla ya viwanda vine (4) vimepigwa faini ya shilingi milioni 80 kutokana na kuzalisha mifuko ya plastiki isiyo na ubora.
Hii ni hatua ya muendelezo wa uamuzi wa serikali wa kutekeleza kanuni mpya za udhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki za mwaka 2019 na matumizi ya mifuko mbadala zilizoanza kutumika Juni 01, mwaka huu kwa lengo la kutunza mazingira.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa