Kaimu Afisa Sheria wa halmshauri ya mji Newala ndg. Reginald Mbonde ametoa mafunzo ya usimamizi wa sheria kwa Baraza jipya la ardhi kata ya mkunya na kuwataka kujiepusha na rushwa na upendeleo katika maamuzi.
Mafunzo hayo yamefanyika jana Jumatano 02/05/2020 kwenye ukumbi ya mikutano wa ofisi ya Kata hiyo, ambapo amewataka kusimamia haki katika usuluhishi wa migogoro itakayo jitokeza pamoja na kujiepusha na rushwa ambayo imeonekana kuwa ni changamoto na kulalamikiwa kwenye mabaraza mengi.
Aidha Mbonde amewaeleza kuwa baraza hilo sio chombo cha kutoa hukumu bali lipo kwa ajili ya kushauri na usuluhishi kwa lengo la kutatua migogoro kwenye jamii pasipo upendeleo na ukandamizaji wa haki, na kwamba watausika na usuluhishi wa mashauri madogo wasiyozidi malalamiko ya shilingi milioni tatu.
Hata hivyo amewataka kuwa wasiri na wavumilivu katikautendaji wao kazi kwa kuwa kazi ya utoaji haki haikosi malalamiko kwa kuwa mlalamikaji na mlalamikiwa wote wanaona wapo kwenye nafasi ya kuwa anastahili kupewa haki.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bi. Rehema Bakari Antukene amesema ana imani wa wajumbe wa baraza hilo kwa kuwa wote wamechaguliwa kwenye vijiji vyao hivyo wameaminiwa kusimamia maamuzi kwa kutumia busara walizonazo.
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo Bi. Amina Fumo na Hamisi Akili, wamewashukuru maafisa hao kwa hatua ya kuwapatia mafunzo ya awali kabla ya kuanza kazi na kuielezea kuwa imewaongezea uelewa na ujasiri katika jukumu lao.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa