Baraza la bajeti halmashauri ya mji Newala limeketi februari 3 na 4, 2020 na kupitisha rasimu ya bajeti ya mapato na matumizi ya shilingi bilioni 14.8 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Kwenye rasimu hiyo ya bajeti, imependekeza halmashauri kukusanya shilingi bilioni 2.004 kupitia vyanzo vyake ambapo mapato na matumizi kwa vyanzo vya ndani ni shilingi bil. 1.29 na mapato lindwa ni shilingi milioni 711.3
Aidha fedha za bajeti zilizosalia ni kutoka kutoka serikali kuu, wahisani na wadau wengine wa maendeleo na fedha hizo kwa ujumla, zitatumika kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, kulipa mishahara ya watumishi pamoja na matumizi ya kawaida.
Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Mhe. Sambili Mohamedi ametoa wito kwa kila mmoja anayehusika na na bajeti hiyo kuhakikisha anasimama imara katika kufanya wajibu wake, ili kufikia lengo la halmashauri la kuitekeleza bajeti hiyo kwa ukamilifu wake.
Naye Mkurugenzi wa halnashauri ndg. Andrew Mgaya amesema, ili halmashauri ionekane inawajibika kwa wananchi wake ni lazima ijipime kwa utekelezaji bajeti yake yenyewe, hivyo ni muhimu kusimamia makubalianao hayo kwa vitendo na kwa ushirikiano.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa