Baraza la Madiwani la halmashauri ya mji Newala jana June 03, 2020 limefikia okomo wake wa kiutendaji baada ya kuhairisha shughuli zake baada ya kuwatumikia wananchi waliowachagua kwa miaka mitano.
Hatua hiyo imekuja katika kikao cha baraza maalumu la madiwani la kufikia maridhiano ya ukomo wa uendeshaji wa shughuli za uwakailishi kutokana na matakwa kisheria ambapo madiwani wote kwa pamoja waliridhia hatua hiyo.
Akiwasilisha azimio hilo katibu wa baraza la madiwani, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndg. Andrew Mgaya amesema sheria inataka mabaraza ya madiwani kufikia makubaliano ya kuahirisha shughuli zake kabla ya Waziri wenye zamana (TAMISEMI) kuvunja mabaraza yote siku 14 kabla bunge la Jamhuri ya Muungano halijavunjwa na hatua hiyo inapisha mchakato wa shughuli za uchaguzi mkuu ili kupata wawakilishi wapya watakao chaguliwa na wananchi.
Akizungumza mara baada ya maridhiano hayo, aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe. Sambili Mohamedi amewashukuru madiwani wenzie kwa uwakilishi wao nzuri kwa kuwa baraza hilo lilifanya kazi kwa kauli moja bila kujali utofauti wao wa uwakilishi wa vyama uliokuwepo kwenye baraza hilo.
Kwa upande mwingine Mhe. Sambili amepongeza ushirikiano walioupata kutoka kwa watendaji wa serikali kuanzia kwa Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi, Wakuu wa idara na watumishi wote kwa kipindi chote cha baraza hilo na kuwataka kuendelea na umoja huo hata kwa wale watakaokuja ili kufanikisha mipango ya serikali ya kuwafikishia wananchi maendeleo.
Naye Mkuu wa wilaya Bi. Aziza Mangosongo amesema mshikamano na umoja ulioonyeshwa na baraza hilo ndio uwakilishi wa kweli kwa kuwa umewezesha kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ufanisi, wamesimamia matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo vizuri hivyo wananstahili pongeza.
Baadhi ya Madiwani waliozungumza katika kikao hicho wameishukuru menejimenti ya halmshauri na baraza lote kwa ushirikiano wao hatua ambayo imewapa uzoefu wa uwakilishi kwa kuwa baadhi yao walikuwa ni wachanga katika uwakilishi wa wananchi hivyo wamejifunza mengi katika kuutumikia umma.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa