Baraza la madiwani halmashauri ya Mji Newala limeridhiria maboresho ya mabadiliko ya sheria ndogo ya tozo ya uingizaji wa mifugo na samaki ndani ya halamshauri hiyo kwa kuongeza ushuru wenye lengo la kuboresha huduma.
Hatua hiyo imefikiwa katika Mkutano wa siku ya kwanza wa baraza la madiwani la robo ya pili Oktoba – Disemba 2019/2020 lililoketi jana Alhamisi Januari 30, 2020, ambapo kwa pamoja baraza limeridhia mabadiliko ya sheria ndogo ya Hifadhi mazingira No.3(2)(C) ya Mwaka 2019 ya halmashauri hiyo kifungu cha 4(1) kwa kuongeza sehemu ya 14 kuhusu kutoza ushuru.
Tozo ambazo zimependekezwa na kuidhinishwa na madiwani hao ni kuingiza ng’ombe 1 gharama ni Tsh. 1,500/=, Mbuzi Tsh. 500, Kondoo Tsh. 500, Samaki tenga/boksi dogo Tsh. 500/=, Samaki tenga/boksi la kati Tsh. 1,000/= na Samaki tenga/boksi kubwa ni Tsh. 2,000/=
Akizungumzia hatua hiyo mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Sambili Mohamedi, amesema lengo la mabadiliko hayo pamoja na kuboresha huduma lakini pia imelenga kuziba mianya iliyopo ya kupoteza mapato ya halmashauri kwa kuwa awali hakukuwa miongozo ya kisheria katika maeneo hayo.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa wialaya Newala Bi. Aziza Mangosongo amewataka madiwani na wananchi kwa ujumla kuwa mstari mbele katika kupiga vita vitendo vya ngono kwa wanafunzi kwani hali ni mbaya hasa kwa watoto waliopo shuleni kuelekea kupoteza ndogo zao.
Mkuu wa wilaya amesema hali hiyo inakua mbaya zaidi kwa kuwa inachangiwa na wazazi wenyewe kwani wengi wanajua kinachoendelea kwa watoto wao lakini hawachukui hatua yoyote na hata pale inapojitokeza watoto wao wamepewa ujauzito hawapo tayari kuwafichua waalifu jambo ambalo kupigwa vita ili kuwalinda watoto.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa