Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeipongeza na kuipatia hati safi halmashauri ya mji Newala kwa usimamizi nzuri wa fedha za serikali na kutekeleza kikamilifu miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Pongezi hizo zimetolewa leo Jumatano Juni 03, 2020 mbele ya mkuu wa mkoa wa Mtwara na Bi. Mary Wembe, Ofisa kutoka Ofisi ya CAG makao makuu katika kikao cha baraza la hoja cha halmashauri hiyo, ambapo katika taarifa yao imeonyesha hoja 18 zilizojitikeza 10 zimeshapatiwa majibu na 8 zilizosalia zinaendelea kupatiwa ufumbuzi.
Mara baada ya kupokea taarifa hiyo Mkuu wa mkoa Mtwara Gelasius Byakanwa, amempongeza Mkuu wa wilaya, mkurugenzi, watumishi, mwenyekiti wa halmashauri pamoja na madiwani kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kikamilifu na kusimamia fedha za umma kwa uaminifu pasipo kujali maslahi yao binafsi na itikadi za vyama.
Aidha amesema mafanikio hayo yanaonyesha wazi kuwa kuna mshikamano wa kiutendaji baina ya ofisi ya mkuu wa wilaya, ofisi ya mkurugenzi pamoja na madiwani kwani hata hoja zilizojitokeza zingine haziusiani na halmashauri na zile za halmashauri zimeshaanza kupatiwa majibu, hiyo inaonesha umakini wa kiutendaji.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Newala Bi. Aziza Mangosongo amesema halamashauri hiyo ni mfano wa kuigwa, kwa kuwa imetekeleza baadhi ya miradi kwa fedha zake za ndani zikiwapo zahanati 4, miradi mingine ni matundu 240 ya vyoo kupitia kapeni ya mkuu wa mkoa ya shule ni choo, madarasa 49 kwa shule za msingi na 30 kwa shule sekondari, mabwalo matatu (3) pamoja na maabara tatu (3).
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Andrew Mgaya amesema katika mapendekezo 18 ya hoja za CAG mapendezo saba tayari zimeshafanyiwa kazi na kufungwa, mapendekezo matatu yamehamishiwa RUWASA na mapendezo mengine nane yapo kwenye hatua za utekelezaji ili kumaliza hoja hizo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Sambili Mohamedi amebainisha kuwa mafanikio hayo, yametokana mtazamo wa kupeleka maendeleo kwa wananchi na kuachana na itikadi za kisisasa ukizingatia halamshauri hiyo ilikuwa na madiwani wa vyama tofauti vya kisiasa na kuwataka hata wale watakao endelea baadae kuendeleza na ushirikiano huo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa