Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Nambunga kilichopo Kata ya Mnekachi Halmashauri ya Mji Newala na kuwaomba wahandisi kuhakikisha wanamaliza ujenzi kwa wakati.
Dkt. Magembe amesema hayo Julai 27, 2022 alipotembelea mradi huo kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo hicho ambapo amepongeza na kuwataka wasimamizi kundeleza juhudi zilizowekwa tangu mwanzo ziweze kukamilisha mradi kwa kuwa fedha za kukamilisha kazi yote zilishatolewa na Mheshimiwa Rais kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo.
Katika hatua nyingine amemuagiza Mganga Mkuu wa Halamshauri kuhakikisha eneo linaliotekelezwa mradi huo linapimwa na kupatiwa hati ya umiliki kwa lengo la kuepusha migogoro inayoyeweza kujitokeza baadae na iweze kusaidia upangiliaji mzuri wa majengo kutokana na eneo lililopo.
Kwa uapande wake Mganga MKuu wa halmashauri hiyo Dkt. Joseph Fwoma amesema fedha zinazotekeleza mradi huo ni jumla ya shilingi milioni 690 ambazo zimetolewa na seriakali kuu kupitia tozo za miamala ya simu shilingi milioni 600 kwa ajili ya majengo ya wagonjwa wa nje (OPD), maabara, jengo la wodi ya kujifungulia na upasuaji, jengo la kufulia, jengo la kumpumzikia wagonjwa pamoja na kichomea taka na shilingi milioni 90 ruzuku ya serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi.
Dkt. Fwoma amesema kituo hicho kinatarajia kuhudumia zaidi ya watu elfu 29 wa kata hiyo na kata jirani kwa huduma za wagonjwa nje, wagonjwa wa ndani na huduma za upasuaji pamoja na kusaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali ya wilaya.
Sambamba na hilo Dkt. Fwoma ameishukuru serikali kwa kuipangatia Halamshauri ya Mji Newala fedha za kutekeleza miradi ya afya kujenga vituo viwili Nambunga na Nanguruwe ukarabati na ujenzi wa majengo mapya katika hospitali ya wilaya ya Newala, dawa pamoja na vifaa tiba.
Dkt. Magembe yupo mkoani mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kutembelea halmashauri zote kukagua na kuona utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika sekta afya na akiwa wilayani Newala ametembelea mradi wa kituo cha Afya Nambunga.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa