Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amesema serikali ipo kwenye maandalizi ya mfumo wa kupima watumishi wanaojitolea ndani ya taasisi za umma ili kuweza kutathmini uwezo wa utendaji kazi.
Dkt. Magembe ameyasema hayo leo Jumatano Julai 27, 2022 mjini Newala akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara kufuatia ombi la mkuu wa wilaya ya Newala Mhe. Rajabu Kundya ayeiomba wizara kutoa kipaumbele kwa watumishi wanaojitolea kwenye kada ya afya serikali hasa katika mikoa ya pembezoni mwa Nchi.
Mhe. Kundya akiwa ofisini kwake amemueleza Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa wapo watu wanajitolea kwa muda mrefu na kufanyakazi kwa uaminifu lakini ajira zinapotoka hawapewi kipaumbele kitu ambacho kinavunja moyo na wakati mwingine wanaopata ajira wanafanya jitihada za kuhama kwa kutokubalina na mazingira.
Dkt. Magembe imekiri uwepo wa changamoto hiyo na kueleza kwamba serikali imelibaini tatizo hilo na tayari imeshaanzisha mchakato wa kuweka mfumo wa kielektroniki utakaowezesha kuwapima ili iwe rahisi kujua uwezo wao kitu ambacho kwasasa hakipo na inamlazimu mtumishi anaejitolea kutumia namba ya utambuzi ya mtumishi aliyeajiriwa kufanyakazi zake.
Hata hivyo amewakata wakurugenzi kuweka utaratibu wa kuwatambua watumishi hao na kupima utendaji wao kazi wa kila siku kupitia mfumo rahisi utakaowezesha kutambua taarifa zao hata inapotokea nafasi za ajira iwe rahisi kupata vielelezo, kwa kuwa watumishi hao ni muhimu kwa kuzingatia hiari yao kufanya kazi wakiwa hawana ajira rasmi.
Naibu Katibu Mkuu yupo mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi kutembelea halamshauri zote za mkoa huu kuona utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwenye kada ya Afya na wilayani Newala ametembelea mradi wa ujenzi Kituo cha afya Nambunga kuona hatua za utekelezaji mradi huo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa