Jamii imetakiwa kutambua kuwa fedha za mfuko wa jimbo ni zipo kwa lengo la kusaidia miradi ya wananchi iliyoanzishwa kwa manufaa ya Taifa ili iweze kukamilika na haipo kwa ajili ya kutekeleza miradi mipya.
Hayo yameelezwa jana Jumamosi July 16 2022, na Mbunge wa jimbo la Newala Mjini ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mh. George Mkuchika, wakati anatoa ufafanuzi wa swali la mjumbe wa kikao maalum cha kamati ya jimbo la Newala mjini cha kuwasilisha utekezaji wa ilani kuanzia Januari hadi Juni 2022, aliyehoji fedha za mfuko huo zinakutekeleza miradi ya wananchi.
Katibu wa CCM kata ya Mahumbika Bw. Ally Mbolele akihoji swali hilo alitaka kujua kwanini fedha za mfuko wa jimbo azifanyi utekelezaji wa miradi katika kata yake na badala yake anasikia kwenye maeneo mengine zikiwanufanisha wananchi.
Akijibu swali hilo Mhe. Mkuchika amesema mfuko huo katika kuanzishwa kwake ulilenga kuchochea maendeleo ya jimbo kwenye miradi iliyoanzishwa na nwananchi wenyewe ambapo wananchi wanatakiwa kuanadika barua ya kuomba kamati isaidie katika hatua ya utekelezaji wa mradi husika.
Aidha ameitaka jamii kutambua kuwa mfuko huo ni kwa ajili ya jimbo lote na hauwezi kuvifikia vijiji vyote ndani ya mwaka mmoja badala yake kamati baada ya kupokea maombi inaangalia baadhi ya maeneo yenye vipaumbele kwa wakatai huo.
Hata hivyo amefafanua kuwa kamati haina jukumu la kuidhisha fedha za mfuko kutekeleza mradi wote bali ni kuunga mkono kwa sehemu fulani na kamati imejitahidi kutenda haki na kwa uwazi, “fedha za mfuko wa jimbo hiendi kutekeleza mradi, inaenda kusaidia mradi ambao tayari umeanza, ule ni mfuko unaita wakuchochea, kakuchochea maendeleo ya jimbo”. Alieleza.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa