Halmashauri ya Mji Newala imetumia shilingi milioni 120 za mapato yake ya ndani, kuanzisha shule mpya ya sekondari katika ukanda wa mto Ruvuma inayotarajia kuanza mwezi Januari mwaka 2023.
Akizungumzia ujenzi wa sekondari hiyo Jumatatu 17 Julai, 2023, Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini Mhe. George Mkuchika amesema halmashauri imechukua hatua hiyo kutokana na kuona adha wanaoipata wanafunzi wanaotoka ukanda huo ambao wanatumia zaidi ya kilomita 10 kufuata masomo.
Mhe. Mkuchika akiwa anaendelea na mikutano jimboni mwake amesema, halmashauri ilishatekeleza sera ya serikali ya elimu ya kuwa na sekondari kwa kila Kata, lakini waliona upo umuhimu wa kuanziasha shule hiyo ili kutimiza ndoto ya elimu kwa watoto zinazokwamishwa na utoro unao tokana na umbali.
“Sisi madiwani tuliona adha wanayopata watoto wakati wa masika na hata umbali ulipo wanapandisha mlima huu kila siku kwenda tu ni zaidi ya kilometa 10 tukasema lazima tuwe na shule ya sekondari huku chini na matokeo yake ndio haya” Alieleza Mhe. Mkuchika
Wananchi wa kata za Nanguruwe, Mcholi 1 na Mkunya wametoa shukrani zao kwa halmashauri, na kupitia taarifa iliyosomwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mcholi 1 Ndg. Bwamkuu Ally, imebainisha katika awamu ya kwanza halmashauri ilitoa shilingi Milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi, nyumba ya mtumishi, pamoja na matundu sita ya vyoo.
Aidha wameeleza kuwa ujenzi wa awamu ya kwanza umekamilika isipokuwa nyumba ya mtumishi ambayo ipo kwenye hatua ya ukamilishaji na awamu ya pili halmashauri imetoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa ambavyo ujenzi wake unakaribia kukamilika.
Hata hivyo akiwa katika vijiji vya Chiunjila, Chihanga na Mapili vijiji lengwa vya shule hiyo walimuomba apendekeze jina la shule ambapo alipendekeza iitwe Benjamini Mkapa Sekondari na wananchi waliridhia pendekezo hilo.
Afisa mipango wa Halmashauri ya Mji Newala Bi. Sophia Makungu amesema halmashauri itaendelea kutenga fedha za mapato ya ndani kutekeleza miradi mbalimbali itakayoibuliwa na wananchi huku akiwasisitiza kuendelea kujitolea wakati wa utekelezaji ikiwa ni sehemu ya mchango wa jamii.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa