Halmashauri ya mji Newala leo Jumanne Mei 26, 2020 imepokea vitambulisho vya wajasiriamali 1200 kwa ajili ya kuanza kuwauzia wajawasiriamali wadogo huku wasimamizi wa zoezi hilo wakitakiwa kujiepusha na ubadhirifu.
Akikabidhi vitambulisho hivyo kwa Afisa biashara wa halmashauri ya mji Newala, Mkuu wa wilaya Newala Bi. Aziza Mangosongo amesema mwaka jana wilaya ya Newala ilifanya vizuri kwenye mauzo, hivyo ni wajibu wa watendaji kusimamia kikamilifu na uadilifu.
Aidha Mhe. Mangosongo amewakata watendaji ambao wanasimamia zoezi hilo kuhakikisha wanatunza kumbukumbu zao vizuri na kuacha kujikopesha fedha za mauzo ili kujiepusha na tuhuma ubadhilifu na matumizi mabaya za fedha za umma.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndg. Andrew Mgaya, mara baada ya kupokea vitambulisho hivyo amewataka watendaji kwenda kuuza vitambulisho hivyo kwa wajasiriamali wadogo pekee kwa kuwa wafanyabiashara wengine wenye namba za utambulisho (TIN) wana utaratibu wao wa kulipa kodi ya mapato.
Hata hivyo ameeleza kuwa sasa hivi serikali imeweka utaratibu nzuri wa malipo hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha fedha zinaelekezwa mahali sahihi, zilipiwe benki kwa kutumia control namba huku akiwaonya wale watakaobainika kufanya kosa la wizi wa fedha watachukuliwa hatua za kiutumishi.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi Ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Newala, Kamanda Edwin Mukama, amesema kazi ya TAKUKURU ni kufuatilia fedha za umma na hizo fedha umma hivyo atakayebainika kufanya kosa, atakuwa ni muhujumu uchumi na kosa hilo halina dhamana na ukibainika mahakani adhabu yake ni kifungo cha miaka 25 hadi 20, hivyo kila mmoja azingatie maelekezo na kujua wajibu wake.
Akimuwakilisha Kamanda wa Polisi wilayani hapa, Mkuu wa kituo cha Polisi Newala SP. Apolinary Mwangailo amesema jeshi hilo halitakuwa huruma kwa wale watakaobainika na makosa, kwa kuwa maelekezo yote yameshatolewa na wajibu sio kuwaonea huruma wafunjifu wa sheria na taratibu.
Zoezi la ugawaji vitambulisho hivyo ni hatua ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwatambua na kuwashirikisha wajawasiriamali wadogo kuchangia maendeleo ya Taifa na mwaka huu 2020 limeigia awamu yake pili vikiwa limefanyiwa maboresho ya taarifa za mjasiriamali, makundi ya wajasiriamali wanastahili pamoja fumo wa malipo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa