Halmashauri ya Mji Newala kwa mwaka 2024/2025 imetekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo jumuishi ya asilimia 10% yenye thamani ya shilingi milioni 292.8 kwa makundi lengwa ya vijana, wanawake na makundi maalum.
Mkuu wa Wilaya ya Newala Alhaj. Mwangi Kundya, akiwa katika hafla ya kukabidhi hundi mfano kwa vikundi vya wajasiriamali, ameipongeza halmashauri hiyo kwa kutekeleza sera hiyo iliyolenga kuinua mitaji na kuwaongezea mapato wafanyabiashara wadogo.
“niwapongeze kutenga fedha na pia kuwaibua wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika kuwekeza katika shughuli mbalimbali za kibiashara ili kujipatia mapato ni Imani yangu fedha hizi zitaendelea kufanyakazi kama zilivyo kusudiwa”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndg. Geofrey Nnauye amesema mfumo jumuishi wa utoaji mikopo 10% kwa kushirikiana na baki upo kwenye matazamio, hivyo vikundi vinapaswa kutekeleza makubaliano ili kuleta ufanisi.
“Halmashauri ya Mji Newala tuanatoa mikopo kwa kushirikiana na benki ya NMB, kwasababu tumeingia kwenye mabadiliko haya niwaombe yale mazoea ya kule nyuma ya ukusanyaji na urejeshaji wa fedha tubadilike tusije kuukwamisha mpango wa taifa”,
Naye Afisa maendeleo ya jamii wa Mkoa wa Mtwara Bi. Thabitha Kilangi ameiomba banki ya NMB pamoja na maafisa maendeleo wa halamshauri kuendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali hao kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili wakue kiuchumi kutokana na shughuli zao.
Afisa Maendeleo ya jamii wa Mji Newala Bi. Joyce Israel ameeleza kuwa 2024/2025 kulikuwa na maombi ya mkopo kutoka kwa vikundi 115 na baada ya kamati za uhakiki vikundi 89 vilihidhinishwa kupata mkopo.
Aidha Israeli amefafanua kuwa, Vikundi 60 vimepokea fedha shilingi milioni 292.8 kwa awamu ya kwanza 33 vikiwa vya wanawake, 13 vya vijana na vikundi 9 vya watu wenye ulemavu huku vikundi 29 vilivyobaki vitapokea shilingi milioni 59.2 katika robo ya pili ya 2025/2026.
Meneja wa mauzo kanda kusini wa benki ya NMB Ndg. Frank Njawala akimwakilishi meneja wa kanda hiyo amesema kipaumbele kimojawapo cha benki yake ni kuwafikia wafanyabiashara wadogo hivyo wamejipanga kushirikiana nao mpaka wafikie hatua ya mafanikio.
Hata hivyo Njawala amefahamisha kuwalinda wafanyabiashara wadogo kwa kuwa tafiti za jukwaa la Uchumi duniani zinaonesha biashara ndogo zinachangia nusu ya pato la taifa pamoja na kuongeza ajira kwa wastani wa 80% ya ajira zote kwa nchi za afrika.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa