Halmashauri ya Mji Newala imeibuka mshindi wa tatu katika sanaa ya muziki wa asili na kuzawadiwa kikombe katika mashindano ya kitaifa ya mamlaka za serikali za mitaa (SHIMISEMITA).
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Geofrey Nnauye amempongeza afisa utamaduni wa halmashauri hiyo Ndg. Faraji Hamisi kwa kazi kubwa aliyoifanya ya uwakilishi wake kupitia kuimba muziki hadi kufikia ushindi huo.
Adha Ndg. Nnauye amesema watumishi wajiandae kwa ajili ya mashindano yajayo “Nakupongeza afisa utamaduni wetu Mr. Faraji kwa kazi nzuri, mwaka huu umepita naomba kwa pamoja tujipange kwa ajili ya mwakani”.
Naye afisa utamaduni ameeleza kufurahishwa kwake kwa ushindi waliopata huku akifafanua kuwa wameshinda kupitia uimbaji wa mziki wa asili wa singeli.
Mashindano ya SHIMISEMITA ngazi ya taifa yamehitimishwa Agosti 29, 2025 jijini Tanga ambapo yalihusisha michezo mbalimbali pamoja na mashindano ya sanaa na mwaka 2026 yamepangwa kufanyika jijini Mbeya.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa