Watendaji wa Serikali ngazi ya Kata na Vijiji wa halmashauri ya Mji Newala wametakiwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa kuishirikisha jamii ya maeneo husika kwa kuwa wao ndio wanufaika wa moja kwa moja hivyo inawapasa washiriki kwenye hatua za utekelezaji.
Wito huo umetolewa jana Alhamisi Julai 16,2020 na Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo wakati anahitimisha ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa matundu ya vyoo katika halamshauri hiyo kupitia kampeni ya shule ni choo iliyoasisiwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara.
Mhe. Mangosongo ameipongeza hatua iliyofikiwa na halamashauri hiyo kwa kujenga matundu 240 ya vyoo tangu kuanza kwa kampeni hiyo lakini amewakosoa baadhi ya Watendaji wa Kata na Waratibu Elimu Kata, kwa kutosimamia kikamilifu zoezi hilo na kusababisha ucheleweshaji wa kukamilisha mradi katika maeneo yao.
“Huku ambako jamii imeshiriki vizuri miradi imekamilika vizuri lakini huku ambako jamii haijashiriki miradi imesuasua, kuna maeneo waratibu elimu alifika mara moja tu mpaka mradi unakamilika hapo jamii itahamasika vipi? ni lazima musimamie miradi yote inayokuja katika maeneo yenu kwa kuwashirikisha wananchi”, alifafanua Mkuu wa Wilaya.
Hata amewataka watendaji ambao hawajafanya vizuri kwenda kufanya maboresho ya maeneo ambayo hayajakaa vizuri ili kuikamilisha miradi yao huku akisisitiza kuishirikisha jamii na yenyewe ishiriki kuchangia miradi hiyo pamoja na mingine inayojitokeza kwa kuwa wao ndio wanufaika wakubwa.
Kwa upande wake Ofisa Elimu Sekondari wa halamshuri hiyo Mwl. Athumani Salumu, amesema kuwashirikisha wananchi kwenye kuimarisha miundombinu ya shule sio kosa jambo hilo lipo kisheria, waraka namba 3 wa mwaka 2006 wa elimu msingi bila malipo, umeruhusu jamii yote kuchangia kuboresha miundombinu ya shule hivyo pale palipo na maradi wanachi washirikishwe.
Naye Ofisa Elimu Msingi Mwl. Mohamed Mwende, amesema lengo la halamshauri ni kumaliza tatizo la matundu ya vyoo hivyo nimatarajio yao mpango huo utafanikiwa kuwa serikali imewapunguzia mzigo mkubwa kilichopo ni kujipanga kikamilifu ili kukalisha azma yao na ni imani yao watafanikiwa.
Kampeni ya shule ni choo imeasisiwa na Mkuu wa Mkoa Mtwara Gelasius Byakanwa, na inatekelezwa katika mkoa wote wa Mtwara ikilenga kuondoa tatizo la matundu ya vyoo kwa walimu na wanafunzi wawapo shuleni, kuwaondelea adha na kulinda afya zao, ambapo wilayani Newala mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ndiye anayewezesha vitendea kazi kwenye shule zinazotekeleza kampeni hii.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa