Wananchi wenye matatizo ya kiharusi, mifupa na watoto waliochelewa katika hatua za ukuaji wa halmashauri ya Mji Newala mkoani Mtwara wametakiwa kutowaficha wagonjwa na badala yake wajitokeze kupata matibabu kwa njia ya mazoezi.
Wito huo umetolewa na mtaalam wa viungo katika Hospitali ya wilaya Newala Ndg. Markus Lugenge ambaye amebainisha kuwa serikali imeshaleta vifaa tiba hospitanini hapo na tayari huduma imeshaanza kutolewa.
‘’Huduma yetu tumeanza pale ambapo vilipofika vifaa, huduma hii inahusisha wale watu wenye matatizo ya stroke yaan kiharusi, watu wenye shida ya mgongo, kiuno hadi kwenye shingo pia wanaosumbuliwa na shida mbalimbali katika miguu na kushindwa kutembea na watoto ambao wamechelewa hatua za ukuaji”. Ameeleza
Lugenge amesema serikali imetanua wigo wa upatikani wa huduma hiyo ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma karibu na maeneo yao kwa kuwa awali huduma hizo zilikua zinatolewa kwenye hospitali bingwa, za kanda, mikoa pamoja na baadhi ya hospitali za wilaya.
Hata hivyo mtaalam huyo amesema watu wenye changamoto hizo wasipopata ufumbuzi wa shida zao hali ya utegemezi inaongezeka kwenye jamii hivyo ni wakati wa kuchukua hatua ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kuwapatia matibabu sahihi.
“Kama kuna watoto wamepata matatizo ukubwani au walizaliwa na hiyo hali, ningependa kuwahusia wananchi kuwa wasikae nyumbani na watu wenye matatizo ya viungo kwani matatizo kama haya yanaongeza utegemezi katika jamii’’. Amefafanua mtaalam huyo wa viungo
Aidha kwa uapande wake Bi. Mariam Mnemwa mmoja wa wananchi wanaopata matibabu hayo ameishukuru serikali kwa kusogeza karibu huduma ya mazoezi kwakuwa walikuwa wanasafiri kwenda hospitali ya Ndanda au Mtwara ambako walikuwa wanatumia gharama kubwa za usafiri, malazi pamoja na chakula.
“Huduma hii walipotusogezea karibu tunaishukuru serikali kwasabu kila wakati tulikuwa tunaipata mbali tunapata shida pakulala pia nauli unaweza kwenda kwa mwezi mara moja au mara mbili kwahiyo serikali S izidi tu kutuongezea vifaa’’. Alieleza Bi. Mariam
Hospitali wa wilaya ya Newala ambayo ipo chini ya Halmashauri ya Mji Newala ilianza kutoa huduma ya mazoezi kwa wagonjwa wa viungo mwezi Aprili, 2025 mara baada ya kupokea vifaa tiba kutoka serikali kuu.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa