Idara ya elimu sekondari halmashauri ya ya Mji Newala imepokea vitabu 8150 vya masomo ya sanaa na sayansi ikiwa awamu ya pili mgao wa vitabu kutoka wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Akiongea mara baada yakupokea vitabu hivyo na kuvigawa kwa wakuu shule Mei 25, 2022 Mkuu wa idara ya elimu sekondari halmashauri hiyo Mwl. Athuman Salum ameishukuru serikali kwa kutekeleza kwa vitendo utoaji wa rudhuku ya uendeshaji ya 50% ambayo serikali iliahidi kuwa itaelekeza kwenye usambazi ya vifaa vya kufundishia shuleni.
Hata hivyo Mwl. Salum amewataka wakuu wa shule kuvigawa vitabu hivyo kwa walimu wa wasomo ili wanafunzi wavitumie kwa kujisomea na kuongeza ufaulu kwenye mitihani yao kwa kuwa serikali imetekeleza wajibu wake na jambo lililobaki ni wanafunzi kunufaika.
Aidha Mkuu huyo amefafanua kuwa vitabu nilivyopokelewa ni vya masomo ya Fizikia, Jografia, Hesabu, Kemia, Baiolojia, Uraia pamoja na Kiswahili ambavyo kwa masomo ya sayansi zinaenda kupunguza uhaba wa vitabu kwa wastani wa kitabu kimoja kwa wanafunzi 2 na kwa masomo ya sanaa wastani wa kitabu kimoja kwa watoto 4 tofuti na hapo awali ambao ilikua kitabu kimoja kwa watoto 6.
Akiongea kwa niaba ya wakuu wa shule waliopokea vitabu hivyo Mkuu wa shule ya sekondari Newala Mwl. Briton Limbe, amesema vitabu hivyo vinakwenda kupunguza changamoto ya ukosefu wa vitabu shuleni baada ya kubalika kwa mtaala, shule zilikosa vitabu na walimu kwa uapande mwingine walilazimika kutumia njia za TEHAMA kuvitafuta mtandaoni.
Mwl. Limbe amewataka wanafunzi kuchukua hatua za maksudi katika kuongeza juhudi kwenye kujifunza na kujisomea kwa kuwa serikili inatekeleza jambo hilo huku ikimlenga mwanafunzi katika kumuandalia mazingira bora ya wao ya kupata elimu.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa