Kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Halmashauri ya Mji Newala kwa kushirikiana na wataalam wa idara ya afya imeeleza kuwa imejipanga kutoa elimu kwa wanafunzi mashuleni ili kuwaokoa na ongozeko la wahanga wa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Mpango huo umeelezwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Hamisi Namata Makamu mwenyekiti wa Halmashauri na diwani wa Kata ya Mtonya Jumatatu Julai 24, 2023 wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa kamati robo ya nne 2022/2023 ambapo amaesema kamati aimebaini wanafunzi wa shule za sekondari na msingi baadhi yao wameshaanza kujihusisha na ngono wakiwa shuleni.
Namata amesema hali yakuonesha wanafunzi wanajihusisha na ngono inaleta hatari kwa kizazi cha kesho hivyo ni lazima elimu kutoka kwa wataalam iwafikie mapema waweze kutimiza ndoto zao kwa kujiepusha na mimba za utotoni pamoja na magonjwa ya zinaa.
“Kama halmashauri kupitia idara ya afya tumeendelea kujipanga kutoa elimu kwenye redio, na tumezihusia asasi zote tunazoshirikiana nazo wajipange waandae ratiba waende mpaka mashuleni kuongea na wanafunzi sisi ajenda yetu ni kutoa elimu kwa jamii”. Aliieleza Mhe. Namata.
Aidha amesema lazima
Kwa uapande wake kaimu Mratibu wa Udhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi Halmashauri ya Mji Newala Bi. Regina Likwama amezishukuru asasi zinazojihusisha na mapambano ya kudhibiti ukimwi ndani ya halmashauri kwa kuwa zimekuwa msaada mkubwa katika kuifikia jamii.
Hata hivyo Likwama ameitaka jamii kuzipa ushirikiano asasi hizo zinazosamba vitepe ya kupimia kwa kuwa zinatambuliwa na pia kuacha tabia ya kukimbia kupokea majibu yao baada ya kupima kwa kuwa yana faida kwa aliyepata maambukizi na asiyepata.
“Nawasahuri watu kwanza kujitokeza kupima kama hivo hizo asasi zinasambaza vitepe wapimeee.. na wale wanaobainika kuwa na virusi vya ukimwi waanze dawa mapema ili wasiweze kuambika wengine”. Alisisitiza kaimu mratibu huyo
Akiongea mwakilishi wa asasi hizo kutoka asasi ya COME amesema wao wanatoa vipimo vya viashiria hivyo ni muhimu kukawa na ufuatilaji wa ukaribu wa watu wanaopimwa na kukutwa viashiria ili wapate vipimo kamili vitakavyo toa uhakika na kuanza kupata matibabu.
Kamati ya kudhibiti Ukimwi halmashauri ya Mji Newala mpaka sasa anashirikiana na asasi tano katika kukabiliana na maambukishi na kuwahudumia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi asasi ya COME, asasi ya KONGA, asasi ya WAZEE, asasi ya VIJANA pamoja na asasi ya WALEMAVU.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa