Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya mji Newala imeitaka jamii kuongeza kasi ya mapambano ya vita dhidi ya maradhi hayo na kupunguza maambukizi yake kwa kupinga vitendo vya usagaji na ushoga hasa kwa wanafunzi na watoto.
Akiongea wakati anafunga kikao cha Kamati hiyo cha robo ya tatu 2022/2023 kilichofanyika Alhamisi Aprili 19, 2023 Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Hamisi Namata amesemani wakati wa jamii kuboresha malezi ya watoto kwa kukemea vitendo hivyo.
Aidha Mhe. Namata ameongeza kuwa hakuna Taifa madhubuti la kesho kama hakuna malezi bora ya watoto “Tunaiomba jamii iwe sehemu ya walimu, jamii iwe sehemu ya wachunga, jamii iwe sehemu ya malezi hawa ni watoto wetu wakiharibika tunahiaribu jamii ya kesho, maana miongoni mwao ndtio tunatarajia tutapata viongozi, miongoni mwao tunategemea tutapata watumishi, Mashekhe, tutapata mapadre, tutawapata watu wa kila aina ambao leo hii wapo kwenye jamii wanatuongoza”.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka dawati la Jinsia Newala Tumaini Ngwanda amesema jamii ni lazima ichukue hatua zamaksudi kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kwa kuwa wao ni wahanga wa kwanza wa vitendo hivyo.
Aidha Ngwanda ameongeza kuwa wapo baadhi ya vijana waliopo shuleni wameibua tabia ya kutaka kufanya mapenzi ya jinsia moja na watu wanaobainika au kuhisiwa kuwa na tabia hizo ambao baadhi yao tayari wamesha athirika na virusi vya UKIMWI.
“Wapo baadhi ya watu ambao tumewabaini kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja na waneleza wazi kuwa wapo wanafunzi wa sekondari wanaowafuata wakitaka kufanya nao mapenzi ya jinsia moja pasipo kujua wao tayari wana VVU, kwa kweli tuwe macho Taifa la kesho kupitia watoto wetu litaangamia”. Alieleza Ngwanda
Mussa Mnuvi mwakilishi kutoka chama cha watu wenye walemavu Newala ameiomba kamati hiyo wataalam wa Afya kuwafikia walemavu kuwapa elimu ya kujikinga namaambukizi kwa kuwa kundi hilo halizingatiwi lakini maambukizi hayachagui kundi Fulani la watu.
Kikao cha kamati ya kudhibiti UKIMWI kiliketi kujadili shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi 20233.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa