Wajumbe wa kamati ya lishe halamshauri ya mji Newala wametakiwa kutambua wanalo jukumu kubwa la kuisaidia jamii ipate uelewa wa kutosha ili iondokane na matatizo ya watoto kupata utapiamlo, udumavu, mgongo wazi na wajawazito kupata kinga wakati wa kujifungua.
Hayo yameelezwa Jumatano Julai 22,2020 na Mwenyekiti wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Bw. Kalistus Komba cha kikao robo ya nne 2019/2020 ambapo amewasisitiza wajumbe kushirikiana kutoa elimu jamii kwa kuwa lishe ni eneo nyeti linalochangia ustawi wa Taifa kwa kuwa na nguvu kazi imara inayotokana afya bora.
Afisa Lishe wa halamashauri hiyo Ndg. Enos Kuzenza amesema halamshauri imeendelea kupata mafanikio katika kugawa vidonge vya FEFO kwa wajawazito na kufikia 85% ambapo kwa robo ya tatu ilikua 80% na utoajia elimu ya unasihi wa ulishaji kwa wazazi wenye watoto miezi 0-23 kwa watoa huduma za afya ngazi ya jamii (CHWs) umefikia 22% kutoka 5% robo iliyopita ambapo watu 1136 wamepatiwa elimu ambapo waliotaraji.
Aidha ameyataja mafanikio mengine kuwa ni kuvuka malengo na kufikia 117% ya kutoa elimu ya uhanisi kwa wazazi na walezi wenye watoto wa miezi 0-23 kutoka kwa watoa huduma za afya ngazi za vituo vya kutolea huduma (HWS) ambapo wazazi 9286 walipata elimu wakati matarajio yalikua 5260 na hiyo imetokana na watoa huduma wa vituo vyote 16 vya halmashauri walipatiwa mafunzo tofauti na robo iliyopita ambayo ni watoa huduma wa vituo vitatu ndio walipatiwa mafunzo.
Kuhusu utapiamlo amebainisha kuwa watoto 21 waliochini ya miaka 5 walibainika kuwa na utapiamlo mkali, 16 kati yao walitibiwa hospitali na kupona na wengine 5 wanaendelea na matibabu nje ya hospitali.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri Dkt. Athanase Emmanuel ameitaka jamii kuachana na mazoea hasa katika matumizi ya chunvi isiyo na madini joto hasa ya mawe ambayo wananchi wengi wanaikimbilia kutokana na urahisi wa bei, na kuagiza kila muuzaji wa chumvi ya mawe ni lazima awe na kibali cha halmashauri ambacho atakipata baada ya chunvi yake kupimwa kiwango cha madini joto na atakaebainika kwenda kinyume atakuchuliwa hatua kali.
Naye Afisa Afya wa halmashauri Bi. Zainabu Iddi ameiomba jamii kuachana na dhana potofu ya kuwazuia wajawazito kutumia vidonge vya FEFO kwa madai kwamba watapata matatizo wakati wa kujifungua jambo ambalo ni upotoshaji na inapelekea kumfanya mama mjamzito na mtoto anayetarajiwa kuwa kwenye hatari kupoteza maisha wakati wakujifungua au mtoto kupata ulemavu.
Wajumbe wa kamati hiyo wamesema wapo tayari kwa pamoja kushirikiana na wataalamu kwenda kwenye jamii kutoa elimu kwa kuwa suala la lishe linaonekana halipewi kipaumbele na wananchi wa kawaida kutokana na kutotambaua athari zinazojitokeza.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa