Kamati ya Lishe ya halmashauri ya mji Newala imeweka mkakati wa kuwafikia wananchi katika maeneo na kuwapa elimu ya lishe ili kukabailiana na tatizo la udumavu kwa watoto wa chini ya miaka mitano hali ambayo hairidhishi kwa ustawi wa watoto.
Mkakati huo umewekwa wakati wa kikao cha kamati hiyo cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika Aprili 14, 2020, ambapo Ofisa lishe wa halmashauri hiyo Enos Kuzenza amesema tatizo la udumavu limefikia asilimia 31.8.
Akizungumza Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mkurugenzi wa halmashauri ndg. Andrew Mgaya amesema katika kukabiliana na tatizo hilo ni lazima kuwe na nguvu ya wataalamu ya kutoa elimu kwa umma juu ya madhara na faida ya lishe bora kwa jamii kwa kwenda vijijini kuzungumza ana kwa ana wananchi.
Aidha ameziagiza idara za Afya, maendeleo ya jamii, kilimo, habari pamoja na utamaduni kuungana na kwenda kuwafikia wananchi katika eneo lote la halmashauri na kuwapa elimu ili kuyafikia malengo ya serikali ya kuondoa utapiamlo na udumavu kwa watoto na kulijenga taifa imara la baadae.
Katika taarifa ya lishe iliyowasilishwa na Afisa lishe imeonyesha halmashauri imefanikiwa katika utoaji wa vidonge vya madini chuma na asidi ya foliki (FEFO) kwa wajawazito 2141 sawa na asilimia 81 kati ya wajawazito 2658 walotarajiwa kupata vidonge hivyo.
Aidha jitihada za udhibiti wa chunvi yenye madini joto zimekuwa na mafanikio kwa kuwa halamashauri imetoa na mafunzo kwa maafisa watendaji ngazi kata na kijiji ya namna ya kuchunguza sampuli za madini joto pamoja na kuwapatia vipimo vya awali vya madini joto kwenye chunvi (Rapid Test Kit RPK) na katika hatua imefanikisha kukamata magari mawili yaliyokuwa yanauza chunvi isiyo na madini joto na kuyatoza faini.
Katika hatua nyingine halmashauri imepanga kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo ili kuongeza nguvu na kuweka kipaumbele katika kuboresha afya ya jamii kwa kubadili mitazamo ya watu juu masuala ya lishe na umuhimu wa jamii kuondokana na utapiamlo pamoja na udumavu.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa