Maafisa ushirika na makatibu wote wa vyama vya wakulima(AMCOS) wilayani Newala Mkoani Mtwara, wametakiwa kuangana na kwenda kusimamia zoezi la uhakiki wa majina ya akaunti za wakulima waliouza korosho ili kurahisisha zoezi la malipo yanyoonekana kwenda taratibu kutokana na kasoro nyingi zinazojitokeza kwenye akaunti hizo.
Maagizo hayo yametolewa leo Alhamis Novembea 29, 2018 na Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo wakati wa kikao chake na makatibu wa Amcos wilayani hapa, kikao kilichofanyika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya mjini Newala, ambapo amesema baada ya kikao hicho viongozi waende moja kwa moja kushirikiana na makarani kutatua changamoto hiyo katika maeneo yao.
Mkuu wa wilaya Newala Mhe. Aziza Mangosongo akitoa maelezo ya msisitizo kwa makatibu wa Amcos Newala.
Mkuu wa wilaya amesema, amelazimika kuwaita viongozi hao na kuwataka kufanya kazi hiyo kutokana na kasoro nyingi zilijitokeza katika kuhakiki akaunti za wakulima, ambapo inaonyesha kuna makosa mengi ya majina jambo linalosababisha usumbufu kwa wakilima kucheleweshewa malipo yao, huku wakiwa na uhitaji wa fedha kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili, “nyie makatibu mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, sasa nyie mnawaacha makarani peke yao, mkae mkijua mambo yakiaribika hamko salama wote mtawajibika msifanye kazi kwa mazoea kwanza nyie wote ni wasomi kuna ambaye sio kidato cha nne kati yenu? ebu wasaidieni wakulima .”amelekeza mkuu wa wilaya.
Hata hivyo Mhe. Mangosongo amevitaja vyama vya Chetu Amcos na Chimale Amcos, kuwa ni moingoni mwa vyama ambavyo majina yote ya wakulima hayako sawa na majina ya akaunti za benki hivyo hakuna mkulima aliyelipwa mpaka sasa, “lakini kutokilipwa huku kwa wakulima ni kwasababu uhakiki wa akaunti haufanyiki au kubebesha mwaka huu hakuna atayelipwa kama amebebesha kila mkulima awe na akaunti yake hakikisheni mnasimamia hilo.” amesisitiza
Baadhi ya makatibu wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na mkuu wa wilaya ya Newala.
Kwa upande wake Afisa Malipo kutoka Banki ya Kilomo ambaye pia Msimamizi wa zoezi la uhakiki Bwana Mauko Madundo amesema mpaka sasa korosho zenye zaidi ya shilingi 1,017,800,000/= (bilioni moja milioni kumi na saba na laki nane) kutoka kwenye vyama 12 zimehakikiwa na fedha zake zipo banki kwa ajili ya amalipo ila kutokana changamoto ya usahihi wa akaunti ni shilingi 698,420,000/= (Milioni mia sita tisini na nane, laki nne na elfu ishirini) ndizo ambazo zimelipwa kwa wakulima wilayani Newala.
Bwana Madundo amesema, hakuna njia ya kukwepa kuwa na akaunti sahihi yenye majina matatu mkulima halisi yanayolingana na akaunti yake, vinginevyo hamna uwezekano wa kufanyiwa malip, hivyo amesisitika suala la kwenda kufanya uhakiki huo haraka huku akifafanua kuwa kigezo cha malipo ya kwanza yanayoendelea ni mkulima kuwa na idadi ya kilo zisizozidi 1500 na kwa wale wenye zaidi ni lazima wafanyiwe uhakiki wa mashamba yao ndipo hatua za malipo zitafuata na uhakiki huo tayari umeshaanza.
“Ndugu zangu kama mnavyojua anae nunua korosho mwaka huu ni serikali, haya ni malipo ya serikali, na endapo hata herufi moja ya jina au namba moja ya akaunti ikikosewa malipo hayawezi kufanyika, hivyo umakini unahitajika sana na changamoto ni hiyo tu ikirekebishwa mambo yataenda vizuri.” alieleza afisa malipo
Viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao hicho wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Newala.
Naye mwenyekiti msaidizi wa bodi ya Chama Kikuu Cha Ushirika Cha Tandahimba-Newala (TANECU LIMITED) Bwana Shaibu Njauka amewataka makatibu kuisaidia serikali kupeleka fedha kwa wakulima kwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kusimamia ubora wa korosho kwa kutoruhusu wakulima kuuza korosho za mwaka jana pamoja na kuwaelekeza kuwa korosho zote zitakaguliwa na kupangwa kwenye madaraja zikiwa galani sio nyumbani.
PICHA ZAIDI
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa