Madiwaniwa Halmashauri ya Mji Newala wametakiwa kuihamasisha na kuisaidia jamii pasipo kujali mipaka ya kata zao kwa lengo la kurahisha kufikia maendeleo kusudiwa ya wananchi.
Hayo yameelezwa leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Yusuph Kateule wakati anafunga kikao cha siku ya kwanza cha baraza la madiwani robo ya kwanza 2021/2022 ambapo amewataka madiwani hao kuwatumikia wananchi kwa kuwa hiyo ndiyo kazi.
Mhe. Kateule amesema ipo dhana imejengeka kwa baadhi ya madiwani kuwa wanatakiwa kufanya kazi eneo fulani jambo ambalo si sahihi kwa pamoja ni watumishi wa wananchi katika halamshauri husika na wanatakiwa kuhamasisha maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halamsahuri Bi. Shamimu Daudi Mwariko amewasisitiza madiwani kuwa mstari wa mbele katika kusimamia maendeleo ya wananchi na hilo ndilo jukumu kubwa na hata baada ya miaka mitano diwani hupimwa kwa usimamizi wa miradi na maendeleo yanayoonekana.
Katika hatua nyingine Bi. Mwariko ameagiza shule zote ndani ya halamshauri zinatakiwa ziwe na mfumo wa kuvuna maji hivyo pamoja na mpango nzuri wa halmashauri wa kuhakikisha kila jengo linakua na kisima, amewaomba madiwani pamoja maafisa watendaji wa kata kwa kushirikiana na shule kuhakikisha wanaweka msisitizo kwenye vikao vya kijamii juu ya kufanikisha jambo hilo, kwa kuwa kwa upande mwingine agizo hilo ni la katibu Mkuu TAMISEMI.
Sambamba na hilo Mkurugenzi ameiomba jamii kwa ujumla kuchukua jukumu la kupambana na tatizo la mimba kwa wanafunzi, shule liwe eneo salama la kuzalisha watoto wa kike kusoma na kuongeza ujuzi na maarifa nisingependa halmashauri yetu iwe sehemu ya kuzalisha watoto wa mitaani.
Naye Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Newala Kamanda Edward Mukama, amesema madiwani wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuisaidia serikali kuzuia ubadhilifu kwa kuisimamia halmashauri ipasavyo katika matumizi yote fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na matumizi mengine.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa