Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2019 Mzee Mkongea Ali, amesema ameridhishwa miradi ya maendeleo ya halmshauri ya Mji Newala na kwamba mbio hizo nitaendelea kumuenzi baba wa Taifa kwa kufanya kazi bila kuchoka, kupinga rushwa kwa vitendo pamoja na kupiga vita ujinga, maradhi na umasikini.
Ameyasema hayo leo Alhamisi tarehe 03/10/2019 alipokuwa anaongea na wananchi wa halmashauri ya mji Newala, waliojitokeza kuupokea mwenge wa Uhuru kwenye maeneo tofauti ya miradi ya maendeleo, nakueleza kuwa serikali imeamua kutekeza hayo kupitia falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu.
Mkongea amesema mwenge wa uhuru unapaswa uenziwe kwa kuendeleza fikra za muasisi wake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyetaka wananchi wote wapate haki zao za msingi kwa kuzingatia nidhamu ya uwajibikaji na uadilifu katika matumizi ya fedha za umma na utumishi bora makazini.
Aidha kiongozi huyo amesema ameridhishwa miradi yote ya halmshauri hiyo ikiwemo klabu ya wapinga rushwa shule ya sekondari Mtangalanga, Zahanati ya Tupendane, Madarasa ya shule ya sekondari Newala, Ujenzi wa barabara ya lami ya kimomita moja (1km), shughuli za vikundi vya ujasiriamali pamoja na utunzaji wa chanzo cha maji cha Mkunya.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Newala mjini ambaye pia ni Waziri wa utumishi na utawala bora Mhe. George Mkuchika amefurahishwa na klabu ya wapinga rushwa kwa kuwa klabu hiyo ni ya wanafunzi na wameokana kuelewa vizuri athari za rushwa hatua ambayo ianaonyesha kuwa itatoa mchango mkubwa wa kupambana na rushwa nchini.
Aidha Mhe. Mkuchika amesema kama nchi itashamiri vitendo vya rushwa haiwezi kuwa na maendeleo kwa kushindwa kukusanya kodi, ndio maana baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani na kudhibiti mianya ya rushwa maendeleo yamekuwa kasi kubwa kwani makusanyo ya uhakika yanafanyika na fedha kupelekwa kwenye miradi ya wananchi.
Hata hivyo viongozi hao kwa pamoja wamewataka wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kujiandikisha, kugombea na kupiga kura kama inavyosisitiza kaulimbiu ya mbio za mwenge 2019 kwa uongozi bora kwenye ngazi ya kijiji, mtaa na kitongoji ndio kiungo muhimu cha maendeleo katika jamii.
Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru 2019 inasema “Maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa”.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa