Mkuu wa wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo leo Novemba 24,2018 amefungua Maazimisho ya miaka 20 ya shirika lisilo la kiserikali la Action Aid na kuwataka kuendeleza ushirikiano na jamii pamoja na serikali katika kuboresha huduma na shughuli za kiuchumi kwa wananchi wanaowazunguka.
Ufunguzi wa maazimisho hayo wilayani hapa, umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya mkuu wa Wilaya ambapo Mhe. Mangosongo amelipongeza shirika hilo katika mambo mbalimbali ya waliyoyafanya ndani ya wilaya.
Aidha Mkuu wa wialaya ameyataja baadhi ya maeneo ambayo shirika hilo wamefanya vizuri kuwa ni uboreshaji ya miundombinu ya elimu kwa kujenga matundu ya vyoo pamoja na kutoa misaada ya madawati kwenye baadhi ya shule, kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi vya akina mama inayosaidi kufikia malengo katika shughuli zao kama za kubangua korosho na mambo mengine.
“lakini niwapongeza Action Aid kwa kufungua chombo kinachowasaidia wananchi kutambua na kupata haki zao hasa wananwake, hivyo niwaombe mkitangaze zaidi ili kiwe kimbilio la wanawake kutafuta na kutetea haki zao.” alieleza Mkuu wa wilaya.
Hata hivyo Mhe. Mangosongo amewaomba kuendeleza ushirikiano wao na serikari ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mh: Rais Dr John Pombe Magufuli . na kuendeleza Kauli mbiu ya “HAPA KAZI TU!!!!!!!!” na huku akiwataka wananchi wa Newala kulitumia Shirika hilo katika kujikomboa kwenye nyanja mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi.
Baadhi ya wananchi waliodhuria ufunguzi huo wamesema Action Aid imewapa mafanikio makubwa katika shughuli zao za kila siku huku diwani wa kata ya Mnyambe Mhe. Sauda Rashidi akieleza kuwa Action Aid ndio waliomjengea uwezo na ujasiri mpaka akafikia hatua ya kugombea nafasi hiyo ya udiwani.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa