Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini Mhe. George Mckuchika amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwapelekea maendeleo wananchi wake.
Ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kuongea na wananchi kupitia mikutano ya hadhara kwenye kata zote 16 za jimbo hilo kuelezea hatua zilizofikiwa za utekelezaji wa ahadi za serikali za kuleta maendeleo kwa watu.
Mhe. Mkuchika ameeleza kuwa ipo miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa na serikali jimboni humo ukiwemo mradi wa ukarabati miundombinu ya maji wenye thamani ya shilingi bilioni 84 pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara ya Mnivata Masasi kwa kiwango cha lami unaogharimu shilingi bilioni 238.
Miradi mingine ni mradi wa usambazaji umeme vijijini REA ambao umelenga kufikisha umeme kila kijiji ifikapo mwezi disemba mwaka huu, ujenzi wa vituo viwili vya afya Nambunga na Nanguruwe ambavyo tayari vimeanza kutumika.
“Kwa hiyo mimi nawaomba watu wa Newala tumpongeze Rais Samia na serikali yake kwa kazi hii nzuri ambayo imeanza”. Alieza Mkuchika
Aidha katika hatua nyingine ameeleza hatua ya utekelezaji wa ahadi yake kuunganisha mji wa Newala na Mkunya kwa lami ambapo amesema kuwa hatua za ujenzi wa barabara ulishaanza na zaidi ya kilometa sita zimeshajenga na hivi karibuni kilometa mbili zingine zitaanza kufanyiwa kazi.
“Mimi katika kampeni ya mwaka 2020 nilisema nipeni miaka mitano nataka niunganishe mji wa Newala na Mkunya kwa lami, tayari nimeanza nimehafikisha lami makondeko na mwaka tumepata lami kilometa mbili tunatoa lami kutoka Makondeko mpaka Kiuta na mwakani tutaitoa Kiuta mpaka kituo cha Afya Mkunya”. Alifafanua mbunge huyo.
Akiwa katika ziara hiyo pia Mhe. Mkuchika alitembelea ujenzi wa kituo kipya cha Polisi Kiuta chenye thamani ya shilingi milioni ya 150 fedha kutoka serikali kuu, ambapo wananchi wa Tarafa ya Mkunya kupitia diwani wao wamemshukuru mbunge jitihada zake za kuiomba serikali kuwapatia kituo hicho.
“Kwa kwali tulikuwa tunapata tabu kupeleka mambo yetu ya kiusalama Polisi kwa kuwa kituo kipo mbali hivyo gharama ilikuwa kubwa lakini ujenzi wa kituo hiki utatusaidia ukizingatia mahakama tayari tunayo hapa hapa tunaishukuru serikali na wewe mbunge kwa kutusemea”. Alieleza diwani wa Kata ya Mkunya Mhe. Karani.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa