Mbunge wa jimbo la Newala Mjini Kapt. Mstahafu Mhe. George Mkuchika leo Jumatano Machi 25, 2020 amekabidhi msaada wa kompyuta 5 na printa 1 vyenye thamani ya shilingi milioni 13.3 katika shule ya sekondari Nangwanda huku akisisitiza kuendelea kusaidia maendeleo ya jimbo hilo kwa vitendo.
Mhe. Mkuchika mbaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumushi wa umma na utawala bora amesema anawashukuru Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) kwa kukubali ombi lake la kupatiwa vifaa hivyo kwa ajili ya wananchi wa jimbo hilo hasa shule hiyo ya wasichana yenye kidato cha kwanza mpaka cha sita.
Aidha amesema yeye kama Mbunge atahakikisha anawasemea wananchi wa Newala kwa serikali na wahisani mbalimbali ili kukabiliana na baadhi changamoto zilizopo na kuweka wazi kuwa ameshaongea na kupatiwa msaada wa madarasa sita na Mamlaka ya Elimu Nchini (TEA) pamoja na madarasa mengine sita kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hata hivyo Mhe. Mkuchika ameeleza kuwa katika msaada wa madarasa sita kutoka mamlaka ya elimu madarasa matatu yatajengwa sekondari ya Nambunga kwa kuwa wanatarajia kuanzisha kidato cha tano na sita kwa wafulana na madarasa mengine matatu tatajengwa shule ya sekondari George Mkuchika na madarasa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu matatu yatajengwa sekondari ya Makote na matatu mengine Shule ya Msingi Nangawala leongo likiwa ni kuongeza madarasa ya shule hiyo na mwakani ianze kupokea wanafunzi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala Ofisa Elimu Sekondari Mwl. Athuman Salum ameshukuru Mbunge kwa msaada huo ambapo amempongeza kwa kuwa mstari wa mbele kuisaidia halamshauri na kwamba hiyo si mara yake ya kwanza na msaada huo utasaidia sana katika hatua za kujifunza na kufundisha kwa wanafunzi na waalimu pamoja na kuondokana na hoja za matumizi ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo FAARS anaohitaji matumizi ya kompyuta.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Mwl. Beatrice Marwa amesema wanamshukuru sana mheshimiwa Mbunge kwa kuwa walikua na uhitaji mkubwa wa kompyuta za waalimu kwa ajili ya kufundishia kwa kuwa malighafi nyingi za kufundishia kwasasa zinapatikana mtandaoni na hata kwa wanafunzi kwa hiyo kwa shule ni ukombozi na kuwaomba wadau wengine wenye uweze wakusaidia wajitokeze kwani bado wanao uhitaji mkubwa wa kompyuta ili kwenda sambamba na mfumo wa elimu yasasa.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa