Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini Mhe. George Mkuchika amesema mshikamano wa wapamoja katika uongozi ndio unaoifanya halmashauri ya mji Newala kuwa halmashauri bora inayoongoza kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ameyaeleza hayo Jumamosi Tarehe 4/12/2021 wakati anahitimisha ziara yake ya siku tatu ya kuongea na wananchi wa kata za Mkulung’ulu, Chitandi pamoja na wakazi wa Newala mjini ambapo amesema umoja wa viongozi ndio siri pekee ya mafanikio ya usimamizi bora wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri.
Mhe. Mkuchika amesema kuwa halmashauri hiyo inafanikiwa kwa kuwa imekua na ajenda moja kuu ya kujadili kitu gani kifanyike kwa maslahi ya wananchi wote, huku akiwapongeza madiwani na mkurugenzi kwa usimamizi na utekelezaji “halmashauri hii wanazungumza na kujadili watu wanataka maji, wanataka barabara, wanataka ukarabati wa shule, wanataka chama cha msingi wanazungumza mambo ya maendeleo, ukienda halamsahauri zingine ni mivutano ajenda moja wanajadili kutwa na kesho inaendelea” amefafanua.
Akielezea mafanikio ya halmashauri ya mji Newala, Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Mhe. Yusuph Kateule amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kuipatia halmashauri shilingi bilioni 1.647 katika kipindi cha miezi sita ili kutekeleza miradi ya Afya, Elimu msingi na sekondari, Barabara, Tasaf na sekta zingine huku akimshukuru Mhe. Mkuchika kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleao.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Alhaj Mwangi Rajabu Kundya amepongeza juhudi za mheshimiwa mbunge kuuboresha mji wa Newala kuufanya kuwa wa kisasa kwa kuwatafuta wadau wa maendeleo wanaowezesha miradi mbalimbali ikiwemo barabara za lami, mataa ya barabarani, ujenzi wa mifereji na mitaro pamoja na mambo mengine yanayopendezesha mji.
Amesema ni viongozi wachache wenye mapenzi ya kweli kwa wananchi wao wanaosimamia shughuli za maendeleo na kuleta matokeo kwani wengine wanashau pale wanapopata nafasi baada ya kuchaguliwa au pale wanapokuwa kwenye nafasi za uongozi.
Katika ziara yake hiyo wananchi wamemshukuru na kumpongeza kwa kazi kubwa alinayoifanya kuifanya halamshauri ya mji Newala kufanana na mji kwa maendeleo yaliyopo katika Nyanja mbalimbali.
Ziara Mhe. Mkuchika ililenga kuwashukuru wananchi wa jimbo la Newala Mjini na kuwaeleza mafanikio na mipango ya maendeleo ya serikali iliyopo katika halmashauri hiyo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa