Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini Mhe. George Huruma Mkuchika amevitaka Vikundi vya ujasiriamali vya walemavu kujitokeza kuomba mikopo ya vijana, wanawake na walemavu inayotolewa na serikali kupitia halmshauri ili waweze kunuifaka nayo na kupiga vita umaskini.
Ameyazungumza hayo mjini Newala siku ya jumamosi 22/02/2020 katika wa hafla ya kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 67.5 kwa vikundi 27 vya vijana wanawake na walemavu viliovyoomba mkopo halmashauri ya mji Newala, ambapo katika taarifa ya utekelezaji ya afisa maendeleo ya jamii ilionyesha uwepo wa uhaba wa vikundi vya walemavu vinavyojitokeza kuomba mikopo hiyo.
Aidha Mhe. Mkuchika ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, amesema utoaji wa mikopo hiyo ni mpango wa serikali na sera ya Chama Cha Mapinduzi, kuendeleza wazo la Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere la kupiga vita ujinga, maradhi na umaskini.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Afisa Elimu Sekondari Mwl. Athuman Salum, amesema tangu halmashauri hiyo ilipoanza kutoa mikopo mwaka 2016/2017 mpaka disemba 2019 imeweza kukusanya zaidi shilingi bilioni 3 na milioni 900 na asilimia 10 ya fedha hizo zimekopeshwa kwa vikundi kama agizo la Mhe. Rais na muongozo wa serikali unavyotaka.
Akiwasilisha taarifa yake Afisa Maendeleo ya Jamii wa halmshauri ya mji Newala Bi. Frola Barakana amesema mpaka sasa jumla ya vikundi 196 na wanavikundi 1648 wameshanufaika na mpango wa serikali wa kuwezesha wananchi kunufaika kiuchumi, kwa kupatiwa mikopo hiyo isiyo na riba ambapo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hadi disemba 2019 halmashauri imefanikiwa kutenga shilingi milioni 360.2 ikiwa ni asilimia 10 ya makusanyo yake halisi na kuelekeza kwenye vikundi vya vijana, wanawake na walemavu.
Sambamba na hilo Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Newala Edwin Mukama, amewataka wanavikundi hao kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za maafisa wanaowadai rushwa wakati wa hatua za kuomba mikopo kwani kufanya hivyo ni kinyume na uwajibikaji wa watumishi na maadili ya kazi yao.
Naye Afisa mwakilishi kutoka Benki ya NMB Bi. Aneth Madiwa amevitaka vikundi kuzitumia akaunti zao benki kwa kuwa hazina tozo za huduma pia zitawasidia kutambua faida na akiba wanayoipata katika mirasi yao sambamba na kuachana na tabia ya kuzitumia kwa kupokelea fedha na kuzitelekeza.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, viongozi wa vijana, wanawake na walemavu wameishukuru serikali kupitia halmashauri pamoja na Mbunge kwa kuwajali na kuwapitia mkopo kwa kuwa inawasidia kutatua changamoto zao za kiuchumia kutokana na faida wanayoipata huku wakivitaka vikundi kusimamia mipango na malengo walioyojiwekea.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa