Mkurungenzi wa halmashauri ya Mji Newala ndg. Andrew Mgaya amewaomba madiwani wa halamsahauri hiyo kutoa uelewa kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yao na kuachana na dhana kwamba miradi hiyo haiitaji nguvu za wananchi.
Ameyazungumza hayo siku ya Jumatatu Aprili 27, 2020 katika mkutano wa baraza la madiwani wa robo ya tatu 2019/2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ambapo mkurugenzi huyo, ameeleza kuwa baadhi ya maeneo wananchi wamekuwa dhana hiyo potofu.
Amefafanua kuwa miradi yote ya mandeleo inahusisha nguvu za wananchi lakini baadhi ya maeneo kwenye mradi wa ujenzi wa madarasa imejitokeza wananchi kukataa kuchangia nguvu kazi wakidai kuwa mradi huo umetengewa fedha za kukamilisha kuanzia hatua za awali hadi kukamilisha jambo ambalo si sahihi.
Akielezea hali ya mapato ya halmashauri mkurugenzi Mgaya ameeleza kuwa hadi kufikia tarehe 30 machi mwaka huu, halmashauri imekusanya shilingi bilioni 1.4 kati ya shilingi bilioni 2.1 sawa na asilimia 69.7 na kujudi zinaendeleza za kukusanya zinaendelea ili kufikia lengo kusudiwa la bajeti.
Aidha katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa Corona amewataka madiwani hao kuwahimiza wananchi kuchukua taadhari kwa kuwa jukumu hilo halina mwenyewe ni la kila mmoja, sambamba na kuwalinda watoto wao kike na mimba wakati wa huu likizo pamoja na kuwahimiza kujisomea binafsi na kupitia runinga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe. Sambili Mohamedi amemuomba mkurugenzi kuwaelekeza watendaji wa halmashauri kutoa ushirikiano kwa madiwani kwani wao ndio chachu ya kutoa msukumo kwa wananchi kushiriki na kusimamia ufanisi wa miradi husika.
Katika hatua nyingine Mhe. Sambili amesisitiza ombi la mkurugenzi kwa madiwani la kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi juu kujitolea nguvu kazi kwa kuwa kutofanya hivyo ni kuikwamisha miradi kitu kitakachopelekea kuzorotesha maendeleo yao wenyewe.
Mkutano huo ulifanyika kwa mda mfupi kwa zingatia tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa kuhusisha watu wachache, kukaa umbali wa zaidi ya mita moja, kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa sabuni maji tiririka.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa