Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala Ndg. Geofrey Nnauye ameishukuru taasisi ya binafsi inayojihusisha na mradi wa kukabiliana na saratani ya matiti ya JHPIEGO kwa kufikisha mradi huo katika halmashauri yake.
Mkurugenzi ameyasema hayo Septemba 10, 2025 wakati anafungua semina elekezi kwa viongozi na watoa huduma ya afya ya msingi kuhusu saratani ya matiti wa halmashauri hiyo “tunashukuru sana kwa mapango huu wa kutupa elimu lakini pia kwenda kwenye ngazi za jamii kuelimishana ili tuweze kutokomeza hili jambo”.
Aidha Ndg. Nnauye ameielezea hatua hiyo kuwa ni muhimu katika kupambana na ugonjwa huo hivyo amewaomba washiriki wa semina hiyo bila kujali jinsi yao kwenda kuielimisha jamii.
Kwa upande wake afisa mshauri wa mradi wa saratani ya matiti (Beat Breast Cancer Project) kutoka JHPIEGO Dkt. Rockfella Elisha amesema wagonjwa wengi wanachelewa kupata matibabu huku wengine kutibiwa kwa waganga wa jienyeji na kusababisha kuongezeka kwa tatizo.
“tunachopata shida ni kwamba watu wengi wanakuja wakiwa wamechelewa, na wanakwenda kuhangaika kwa waganga wa kienyeji, wanakuja hospitali wakiwa wamechelewa sana, kikubwa ni kuwaambia huduma zipo hata hapa hospitali ya wilaya ya Newala”.
Afisa anayeratibu afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Mtwara Bi. Ashura Ausi umesema ugonjwa huo kwasasa unashika kasi na umekuwa wa pili kwa kusababisha vifo kwa magonjwa ya saratani ukitanguliwa na saratani ya shingo ya kizazi.
Hata hivyo ameeleza kuwa mkoa umeona vema uongeze wigo wa mafunzo yasiishie kwa watumishi wa afya bali wahusishe jamii yote kwa lengo la kufanikisha na kurahisisha njia ya utoaji elimu.
Mratibu wa elimu ya afya kwa umma wa mafunzo hayo ambaye ni afisa afya kutoka halmashauri ya Mji Newala Bi. Beatrice Mahiri amesema halamshauri kwasasa ina madaktari na wauguzi wanatoa huduma za uchunguzi wa awali.
Mradi huu wa saratani ya matiti (Beat Breast Cancer Project) mkoani Mtwara unafadhiliwa na Pfizer Foundation chini ya umamizi wa JHPIEGO wakishirikiana na wizara ya afya na wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa ufadhili wa miaka mitatu Januari 2025 mpaka Disemba 2027.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa