Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala Bi. Shamim Mwariko amewaagiza Maafisa watendaji wa kata kuanda mpango wa kutoa elimu ya usalama wa kufunika visima vya maji kwa wananchi ili kuepusha matukio ya vifo vya watoto.
Ametoa agizo hilo Mei 09, 2023 wakati naongea na maafisa hao ofisini kwake kufuatia uwepo wa matukio ya vifo vya watoto wanaozama na kupoteza maisha yao kwenye visima vya maji visivyofunikwa na kueleza hali hiyo haikubaliki katika jamii.
Amesema usalama wa watoto kwenye jamii ni jambo la muhimu, hivyo hatua za kuwalinda watoto lazima zichukuliwe kwenye vijiji na mitaa kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika kwa kuwa baadhi ya wananchi hawajafunika visima vyao na matokeo yake ni mabaya.
Mkugenizi Mwariko ameeleza “na watoto ni wengi sana wanaokufa, tunapokea taarifa hata kutoka maeneo mengine ya nchi yetu, mtoto anapotea watu wanaangaika wanasema sijui amepotea kusikojulikana, kumbe mtoto yupo humo humo nyumbani baada ya siku ngapi mnamuona mtoto amekufa anaelea juu”.
Hata hivyo amesema kwa kuwa sheria ndogo za kuwataka wananchi kuzingatia suala la kufunika visima hivyo zipo basi wale watakaopinga, sheria hizo zitumike kuhakikisha usalama wa watoto kwa kuwa hakuna mbadala wa uhai.
Hata hivyo baadhi ya kata lishachukua hauta ya kukabiliana na tatizo hilo mmoja wa maafisa watendaji Bi. Stephania Muhagama Afisa Mtendaji wa Kata ya Tulindane amesema katika kata yake wameendesha zoezi la ukaguzi na kuwachukulia hatua ya kulipa faini baadhi ya wananchi kwa kuwa elimu ya kufunika visima na matangazo yalishatolewa
Aidha Muhagama amefafanua kuwa lengo lao sio kuwataka wananchi kulipa faini bali ni kuhakikisha usalama wa kimwili na kiafya kwa kuwa hali ya maji kwenye visima visivyofunikwa inaonyesha sio salama kwa matumizi ya nyumbani.
“Maji yale ukiyaangalia tu unajua wala sio salama kwa matumizi ya mwanadamu unakuta maji yana kama ukungu wa kijani umetanda juu na wakati nwingine wadudu wamekufa wanaelea juu ya maji na watu wanayatumia hivyo hivyo, sasa ni vizuri tunachukua taadhari kwa kuwahimiza wananchi kufunika visima.” Alifafanua Bi. Stephania
Wananchi wengi wa Halmashauri ya Mji Newala wamechimba visima vya maji katika makazi yao kutokana na changamoto ya miaka mingi ya upatikanaji wa maji kutokana na wilaya ya Newala kuwa kwenye ukanda wa juu pamoja.
Hata hivyo katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wilaya za Newala, Tandahimba na Mtwara vijiji Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha shilingi bilioni 80 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya maji ya uhakika.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa