Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Newala Mwl. Athuman Salum amebainisha kuwa mafanikio ya ufaulu nzuri kwa matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 umetokana na mbinu ya kufuatilia ufundishaji wa kila siku.
Ameyazungumza hayo ofisini kwake kufuatia matokeo ya wanafunzi wa kidato cha sita ya shule ya sekondari ya wasichana Nangwanda pamoja na Kiuta ambazo zimefaulisha kwa daraja la kwanza na la pili na mwanafunzi mmoja pekee amapata daraja la tatu.
Mwl. Salum amesema matokeo hayo yamewatia nguvu ya kuongeza usimamizi wa ufundishaji kwa kuwa mbinu hiyo ndio iliyoleta matokeo ambayo inamtaka mwalimu kutoa taarifa ya mada alizofundisha kila siku na changamoto alizokutana nazo.
Aidha kwa namna ya pekee amewashukuru walimu kwa utayari waliouonesha wa kupokea mbinu hiyo ambayo amesema anatarajia italeta matokeo mazuri hata katika mtihani wa kidato cha nne wa mwaka huu.
“Matokeo haya hayatokea hivihivi ni kwa juhudi ya halmashauri kupitia idara yetu ya elimu sekondari, tuna program yetu moja yakuhakikisha kilasiku saa 10:00 jioni kunapata ratiba ya shule na vipindi vyote vilivyofundishwa na majina ya walimu waliofundisha kama hajafundisha mimi mwenyewe napiga simu nijue kwanini hajafundisha” Alifafanua Mwl. Salum.
Hata hivyo amesema ipo timu ya uthibiti ubora ya shule ambayo kila Ijumaa inatoa taarifa ya walimu walio wakagua na chanagamoto zilioonekana na mikakati yakukabiliana nazo sambamba na utoaji motisha kwa walimu.
Katika hatua nyingine amewakaribisha wananfunzi wapya wa kidato cha tano wanaotarajia kuanza katika shule mpya za wavulana za Nambunga High School na Malocho High School ambazo zote ni za wavulana na zitakua za mchepuo wa sayansi.
Halmashauri ya Mji Newala ilikuwa na shule mbili za kidato cha tano na sita zote zilikuwa za wasichana na mchepuo wa sanaa na sasa zitaongezeka na kuwa shule nne.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa