Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amewataka wananchi kutambua kwamba, ruzuku ya pembejeo ya zao la korosho inayototelewa na Serikali ni mchango wake katika kumpunguzia mkulima gharama ya uzalishaji wa zao hilo.
Ameyazungumza hayo Jumatano Aprili 03, 2023 katika uzinduzi wa usambazaji na ugawaji pembejeo za korosho kwa msimu wa 2023/24 uliofanyika mkoani Mtwara kwa ajili ya kusambazwa kwa wakulima wa zao hilo kwenye maeneo mbalimbali yanayolima korosho Nchini.
Aidha Kanali Abbas amesema serikali inachangia kwa sehemu lengo ni kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji hivyo ni muhimu kwa kila mkulima kujiwekea akiba ya fedha kwa ajili ya kuongezea ununua wa viuatilifu sokoni ili aweze kutosheleza mahitaji yake.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred amesema kwa msimu wa mwaka huu wamejiwekea lengo la kuangiza tani 49 elfu za Salfa ya unga, viuatilifu vya maji lita Milioni tatu laki moja na elfu thelathini na tisa pamoja na mabomba elfu tano mia mbili.
Hata hivyo Alfred alisema kuwa, “kwa takwimu za mahitaji tuliyonayo ni kwa kwamba viuatilifu hivi ni vingi kuliko mahitaji ambapo kwa wastani wa mahitaji ya salfa kwa takwimu walizokuwa nazo ni kati ya tani 30,000 mpaka tani 35,000 pia ‘’Lengo letu tunataka tujiridhishe katika suala la ubora wa pembejeo kabla ya kusambazwa kwa wakulima na tunaanza kujiridhisha kwa kugawa kwenye maeneo ambayo mikorosho inaanza kuchipua na zitagawiwa kwa wakulima waliyosajiliwa tu ndiyo watakaopewa pembejeo’’.
Aidha, mpaka sasa tayari Tani 8000 za salfa ya unga zimeshawasili Nchini na ambazo zimepokelewa katika ghala la kuhifazia pembejeo la Bodi ya Korosho mkoani humo ni tani 3600, salfa ya unga viuatilifu vya maji lita Milioni moja vilivyopokelewa ni lita laki nane thelathini na sita mia tisa pamoja na mabomba elfu tano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile amesisitiza suala la usimamizi wa ugawaji lifanyike na kila mdau ili wale ambao wana dhamira ya kuharibu utaratibu wa ugawaji wa pembejeo hizo waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Mmoja wa wakulima wa zao la Korosho mkoani Mtwara Bi. Moza Salumu amesema wanaishukuru Serikali kwa kuweka ruzuku kwenye pembejeo kwa kuwa itasaidia kuongeza uzalishaji kutokana na gharama za pembejeo ni kubwa ukilinganisha na mahitaji ya wakulima.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa