Mkuu wa wilaya ya newala Alhaji Mwangi Kundya amesema yapo matukio mengi ya mmomonyoko wa maadili kwa vijana yanayoendelea hivi sasa yanayotokana na ukosefu wa malezi bora.
Hayo ameyaeleza katika kikao cha baraza la wazee mkoa mtwara lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa chuo cha uuguzi na ukunga Newala lililowakutanisha viongozi wa halmashauri 9 wa mabaraza ya wazee ya mkoa huo.
Akifungua mkutano huo akiwa mgeni Mhe. Kundya amesema wazee wanajukumu la kusimamia malezi bora ya vijana ili kupata kizazi salama kwa maslahi ya Taifa.
“mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa vijana na watoto umekuwa ni mkubwa, kiasi cha kulazimika kurudi kwa wazee kuuliza njia. Nyinyi mnaojua njia mtusaidie kujua njia iko wapi?
Mwenyekiti wa baraza hilo mkoani Mtwara Bw. Rashid Kapela ameiomba jamii kuwatambua na kuwatumia wazee katika kutoa mchango wao wa kulisaidia taifa kwenye msingi wa ushauri na kuimarisha maadili.
“Kwahiyo niwaombe nyinyi viongozi mkikuta Kundi la wazee mjue ni hazina na tunu ya taifa, kwahiyo wanashatili kupendwa, kuheshimiwa maana yake usipomuheshimu mzee na wewe baadae hauta heshimiwa”.
Kwa upande wake Katibu wa baraza la wazee Mkoa wa Mtwara Bw. Seifu Chilumba amebainisha kuwa vikao hivyo vinajadili juu ya ustawi wa wazee katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya, uchumi pamoja na mchango wa wazee katika jamii.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho akiwemo mwenyekiti wa baraza hilo halmashauri ya Mji Newala Bw. Omari Chang'anganya wamesema chanzo cha mmomonyoko wa maadili ni utandawazi kupitia mitandao ya jamii.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa