Wilaya ya Newala imepokea Mwenge wa Uhuru 2023 katika kijiji cha Lidumbe Halmashauri ya Mji Newala kwa ajili ya kuanza kufanya shughuli za kukagua, kuzindua, kuweka mawe ya msingi, kuona na kufungua miradi ya maendeleo.
Akipokea Mwenge huo Mkuu wa Wilaya ya Newala Alhaj Mwangi Rajabu Kundya Alhamisi Tarehe 6 Aprili, 2023 kutoka kwa Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe. Patrick Sawala, alisema wilaya ya Newala ina miradi 16 ya maendeleo katika halmashauri zake mbili yenye thamani ya shilingi bilioni 5.82 na utakimbizwa umbali wa kilomita 166.
Aidha Mwenge ukiwa Halmashauri ya Mji Newala umepitia miradi 9 na kuridhishwa na miradi yote ikiwemo ikiwemo kuzindua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Mnaida unaohusisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 225,000 na miundombinu ya usambazaji maji utakaowanufaisha watu 20,547 wa Kata za Mcholi 1 na 2 pamoja na Kata ya Mtumachi wenye thamani ya shilingi bilioni 2.326.
Aidha mbio hizo zimezindua nyumba ya mtumishi wa Zahanati ya Mnaida iliyojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kutumia force account yenye thamani ya shilingi milioni 52.452 ambapo kati ya fedha hizo shilingi laki 5 ni mchango wa nguvu za wananchi.
Kufuatia kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023 isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa” Halamshauri ya Mji Newala kwa kushirikiana na TFS iliunda kuunda klabu ya uhifadhi mazingira shuleni na kuandaa maradi wa upandaji miti 775 yenye thamani ya shilingi milioni 1.212.
Aidha katika kuendelea kusimamia wa kauli mbi hiyo Halmashauri ilikua na maradi wa kikundi cha wajasiriamali wanaojihusisha na ukusanyaji na uchakataji wa plastiki chakavu kilichowezeshwa na halmashauri kununua mashine kupitia mikopo ya 10% wenye thamabani ya shilingi milioni 8, kwa leng kukabiliana na changamoto ya usafi wa mazingira pamoja na kuwapatia kipato.
Miradi mingine iliyopitiwa Mwenye wa Uhuru Halmashauri ya Mji Newala ni Ujenzi wa barabara ya lami ya Chitandi yenye urefu wa kilometa 2 yenye thamani ya shilingi milioni 975, Mradi wa kufungua huduma kituo cha Afya Mnekachi, Mradi ya klabu ya kupinga rushwa shule ya sekondari Makondeko pamoja na ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Mtangalanga yenye thamani ya shilingi milioni 40.
Aidha ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru umewasisitiza wananchi kuwa wazalendo wa Taifa na kuzingatia utunzaji mazingira ili kuondoka na hali mbaya ya mabadiliko ya tabia ya nchi, kuzingatia lishe bora, kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, kujikinga dhidi ya malaria, kupinga rushwa na kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mwenye wa Uhuru 2023, Halashauri ya Mji Newala umekimbizwa umbali wa kilometa 88 katika Tarafa 2, Kata 12, Mitaa3 na Vijiji 20 kisha kukabidhiwa halmashauri ya wilaya Newala.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa