Watumishi wa Halmashauri ya Mji Newala wametakiwa kufanya kazi zao kwa kushirikiana wao kwa kwao pamoja na viongozi wengine ili kurahisisha lengo la serikali la kuwafikishia wananchi maendeleo kwa haraka.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Yusuph Kateule Jumatano Julai 26,2023 wakati anafunga kikao cha kamati ya fedha robo ya nne 2022/2023 na kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa halmashauri hiyo pamoja na Katibu Tawala mpya wa wilaya ya Newala.
Mheshimiwa Katule akiwakaribisha viongozi hao amesema watumishi wa serikali kila mmoja anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uwazi na ushirikiano hali itakayopelekea wananchi kupata huduma bora kutoka kwenye vitengo na idara za serikali.
“Nikushukuru sana Katibu Tawala nikukaribishe Newala pia nikushukuru Mkurugenzi karibu sana sisi tunamatumaini na wewe, watumishi jitahidini kuweka mambo vizuri, muwe na ushirikiano ninyi kwa ninyi na kuweni wawazi ili tuwatumikie wananchi wetu vizuri”. Alieleza Mheshimiwa Kateule
Kwa upande wake Katibu Tawala mpya wa Wilaya ya Newala Ndg. Thomas Safari amesema hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio katika utendajikazi hasa wa taasisi kama halmashauri ni lazima kuwe uwajibikaji wa pamoja kwa kuwa lengo la watumishi wote ni moja.
“Mfano sasahivi mna hivi vishikwambi kuna mambo ya kidigitali lakini je ? ulipoona kasoro kwenye taarifa kama ya ukaguzi ulichukua hatua gani kumuona mkaguzi au kumuambia mwenzako amuone mkaguzi ili kuweka sawa mambo yake.. lazima mshirikiane”. Alifafanua katibu Tawala huyo.
Hata hivyo Katibu Tawala Safari amewataka watumishi kupendana, kushauriana na kukosoana kwa nia njema pale inapojitokeza mwingine amekosea au kuonesha udhaifu katika utendaji jambo ambalo litasaidia kuimarisha sifa ya mtumishi na huduma zinazotolewa na halmashauri.
Akizungumza kwa mara ya kwanza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Geofrey Nnauye ameahidi kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu na kuwasisitiza watumishi kusimamia uwazi na kujituma wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Aidha Nnauye ametaka kila mmoja asimamae kwenye nafasi yake aliyoaminiwa na serikali kutimiza wajibu wake wakiutumishi kwa uaminifu ili kujiweka salama na kuondokana dosari za kunyooshewa vidole au kutiliwa shaka.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa