Mwenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa wa halmashauri ya Mji Newala, walioshinda kwenye uchaguzi uliofanyika Novemba 24, mwaka huu, leo wameapishwa tayari kwenda kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi na serikali.
Hafla hiyo imefanyika leo Jumatano Novemba 27, 2019, kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mwanzo Myambe-Newala Bi. Devotha Salumu, ambaye amewataka kuzingatia viapo walivyokubali kiapo cha uaminifu pamoja na kiapo cha utii na uadilifu.
Akizungumza mara baada wa kuapishwa viongozi hao wapya, Mkuu wa wilaya Newala Bi. Aziza Mangosongo amewataka kutambua jukumu walilonalo ni kubwa hivyo umoja unahitaka ili kufanikisha malengo ya serikali na kuwatumikia wananchi waliowachagua na kuwataka kuondoa makundi yote na kuimarisha umoja baina ya vyama na wananchi wao.
Aidha Mkuu wa wilaya amewata kutokumbatia madaraka na badala yake washirikiane kikamilifu na wananchi wao kupitia vikao halali kuibua na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika mitaa yao na kuepuka kujigeuza miungu watu kutokana na madaraka waliyonayo.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mtwara anayeshughulikia serikali za mitaa Bw. Nuru Ringo amewataka wenyeviti kuzingatia kanuni, kuitisha mikutano ya halamshauri ya mitaa kwa mujibu wa kanuni, kuwapa wananchi taarifa za mapato na matumizi pamoja na kuwa na msimamo wakati wa kusuluhisha migogoro kwa maslahi ya pamoja.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Newala Bw. Mussa Ramadhani Mwevi, amewapongeza viongozi hao, ambao wote wametokana na CCM na kuwataka kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na watendaji wa serikali katika kuwatumikia wananchi na kuachana na kubaguana.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya uchaguzi huo, Msimamizi wa uchaguzi halamashauri ya mji Newala Bi. Sophia Makungu amesema kulikua na vituo 189 vya kupigia kura na vyama vitatu CCM, CHADEMA na CUF vilishiriki uchaguzi huo, huku mitaa miwili pekee ndio ambayo iliingia kwenye mchakato wa kupiga kura na maeneo mengine wagombea wakipita bila kupingwa na kwenye matokeo ya jumla Chama Cha Mapinduzi kimeshida viti vyote.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa