Shule ya Sekondari Newala iliyopo Halmashauri ya mji Newala, imeweka mkakati kufanya vizuri na kuondoa daraja sifuri na kuongeza ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu kwa wanafunzi watakaofanya mtihani wa kidato cha nne na cha pili mwaka huu 2020.
Hayo yamebainishwa leo Jumatano Julai 15, 2020 na Mkuu wa shule hiyo Mwl. Briton Limbe wakati anaelezea mipango iliyokwa na shule yake kwa ajili ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi wanaofanya mitihani, “Sisi kama shule tayari tumeshaweka mkakati wa kufundisha mbinu za ziada kwa masomo ambayo wanafunzi wanayaona ni rahisi ili tuwatie moyo na kuwaongezea maarifa ya kufanya mitihani kwa kujiamini ili waondokane na F”, ameeleza Mkuu huyo.
Amesema wameyaangalia masomo manne ambayo wanafunzi huwa wanayapenda ambayo ni Kiswahili, Kiingereza, Uraia na Historia ambayo kama wakiwajengeza uwezo kikamalifu na kuwaelekeza maeneo muhimu ya kuzingatia, wanafunzi atapata alama nzuri na kuondokana na ziro.
Aidha Mwl. Limbe ameutaja mkakati mwingine ni kuwa na muda ziada wa masomo na kutoa msaada kwa wanafunzi wenye uwezo mdogo, kufanya mitihani kila mwisho wa wiki yenye hadhi ya Taifa ili wanafunzi wapate picha halisi ya mitihani hiyo pamoja na kuhamasisha wazazi kuwahiza watoto wajisomee wakiwa nyumbani na kuchangia chakula ili wapate chakula wawapo shuleni.
Kaka Mkuu wa shule hiyo Ayubu Issa Zefania anayesoma kidato cha nne amesema wao kama wanafunzi wameopokea mkakati huo kwa mikono miwili kwa kuwa wanaamini mwanafunzi akifanya mazoezi mara kwa mara lazima atapata ufaulu nzuri na zaidi wanazingatia nidhamu kwani ndio msingi wa mafanikio yao.
Kwa upande wake Nulfa Omary wanafunzi wa kidato cha pili amesema mkakati huo umewapa hamasa kwa kuwa walikaa muda mrefu nyumbani na muda uliobaki kuelekea kufanya mitihani ni mchache hivyo anawaomba wazazi wawaunge mkono kwa kuchangia chakula ili muda wao mwingi wadumu shuleni kwani ndiko wanakopata msaada wa kieleimu na anaamini wanafunzi wengi wawapo nyumbani hawasoni.
Shele hiyo katika mtihani wa mwaka jana 2019 kitado cha nne ilifaulisha kwa zaidi ya 70% na kidato cha pili zaidi ya 80% na kwenye mkakati wao wasasa wamedhamiria kufikia ufaulu wa asilimia 100%.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa