Halmashauri ya mji Newala yaishukuru Serikali kwa kuwaboreshea mazingira ya kazi kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya kujenga jengo jipya lakisasa la utawala ambalo limeshakamilika tayari kwa kutumika na watumishi wa idara mbalimbali wa halamsahuri hiyo.
Hayo yameelezwa na Mkurugunzi wa halmashauri hiyo Ndg. Andrew Mgaya katika hafla ya kukabidhiwa jengo, iliyofanyika leo Jumatatu tarehe 10/02/2020 katika ukumbi wa ndani wa mikutano wa jengo hilo, ambapo amesema hiyo ni hatua kubwa ya kujivunia kwa kuwa itaongeza chachu ya utendaji kazi kwa watumishi.
Aidha Mgaya ameishukuru serikali kupitia Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuipatia halmashauri hiyo fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwa pamoja na fedha zilizojenga jengo hilo shilingi bilioni 2.646, na kufafanua kuwa mambo yote yanajieleza yenyewe kwa matokeo yake.
Hata hivyo amemshukuru mkandarasi SUMA JKT Kanda ya Kusini kwa kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu na uvumilivu kwani hata pale zilipojitokeza changamoto mbalimbali bado waliendelea kutekeleza makubaliano kwa kufanya kazi.
Akizungumza wakati anakabidhi funguo kwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo, meneja wa SUMA JKT Kanda ya Kusini Meja Atupele Mwamfupe, amesema haikua kazi rahisi kukamilisha kazi hiyo na udongo na mchanga kupatikana mbali na eneo la mradi kwani udongo na mchanga unaopatikana eneo hilo haufai kwa ujenzi wa maghorofa.
Aidha ameziomba taasisi binafsi na za umma pamoja na halmashauri hiyo kuwaamini na kuwapa miradi kama ya maji, majengo, barabara na miundombinu yake na hiyo itakua na faida kubwa kwao kwenye majanga ya dharula na hata kwenye masuala ya ulinzi na usalama.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe. Sambili Mohamedi baada kuabidhiwa funguo za jengo hilo kama ishara ya makabidhiano rasmi, ameshukuru mkurugenzi, madiwani na watumishi kutobadilisha matumizi ya fedha za zilizotolewa na hatimae kufanikiwa kukamilisha mradi salama na kuielezea hatua hiyo ni kipekee na imetokana na ushirikiano wa pamoja.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Newala, Jabiri Mtanda hayo ni matokeo ya utekelezaji wa ilani ya chama na ahadi zake kwa wananchi na hilo linatokana na usikivu wa viongozi waliopewa dhamana na chama hicho ukianzia kwa Rais Dkt. John Magufuli mpaka mbunge wa jimbo la Newala Mjini Kapt. George Mkuchika ambaye amekua msaada mkubwa kwa maendeleo ya Newala.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa