Mkuu wa Idara ya Kilimo Halmashauri ya Mji Newala Ndg. Kalistus Komba amesema katika kusherehekea sikukuu wa wakulima (Nanenane) Mwaka huu wamejipanga kutoa elimu na maarifa kwa wananchi yatakayowawezesha kubadilisha mitazamo yao.
Ameyazungumza hayo akiwa kwenye viwanja vya maonesho kanda ya kusini Ngongo-Lindi na kubainisha kuwa, kwa kwaka huu wameandaa teknolojia rahisi ya uzalishaji samaki itakayowawezesha wananchi kwenda kufanya ufugaji mpaka wa samaki 200 katika eneo dogo na hiyo itawanufaisha watu.
Aidha Ndg. Komba ameeeleza kuwa halmashauri imeongeza huduma za elimu kwa kuongeza vipando vya mazao mbalimbali pamoja na kupeleka wajasiriamali 23 ambao wanawezeshwa na halmashauri katika shughuli zao hivyo watasaidia kuwajengea uwezo watu wengine.
Hata hivyo amewata wakulima na wananchi kuyatumia maonesho hayo kwenda kujifunza na kuzijua fursa zingine ambazo ni kama chachu ya kuongeza uzalishaji na kukuza mnyororo wa thamani wa shughuli za kilimo na ufugaji unaokwenda sambamba na masoko ya bidhaa za kilimo.
Mkuu huyo wa idara ya kilimo amesema kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Wanawake na Vijana ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula”, mwaka huu wamepeleka kikundi cha vijana kilichokopeshwa trekta na halmashauri kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na hiyo inaonyesha ni jinsi gani halmashauri ilishaona umuhimu wa vijana kwenye shughuli za kilimo.
Komba amesma serikali inaamini wanawake na vijana ni nguvu kazi hivyo wahamasike katika kufanya shughuli za kilimo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na chakula kwa wao binafsi pamoja na kuyafikia malengo ya serikali.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa