Vijana na wanawake wajasiriamali waliopo Halmashauri ya Mji Newala, wametakiwa kufungua fikra zao na kuziona fursa zenye tija kwa Taifa zitakazoweza kuwaunganisha na kuwasaidia kufanya mambo makubwa kwa kuwa muelekeo wa Serikali kwasasa ni kutoa mikopo ya mamilioni ya shilingi kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu.
Rai hiyo imetolewa Jumatano June 08, 2022 na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Shamim Mwariko wakati wa ufunguzi wa kikao cha kuwawezesha vijana kutambua fursa za kilimo na biashara na fursa zingine zilizopo kwa vijana ili kuziunganisha na mikopo inayotolewa na serikali kupitia Halmashauri.
Mkurugenzi Mwariko amewataka vijana kubalisha mtazamo wa kuchukua mkopo wa fedha ndogo kisha kugawana na kuchangishana wakati wa marejesho kwa kuwa hilo sio lengo la mikopo hiyo na kwa utaratibu huo nchi haiwezi kukuza uchumi wake.
Amesema vijana na wanawake wanatakiwa wachukue mikopo itakayo wanuafaisha wao wenyewe na ikiwezekana itoe ajira kwa wengine ili jamii yote inufaike, “baadhi yenu humu wamepokea mikopo ya milioni ishirini, baadhi yenu wamepokea mikopo ya milioni kumi na baadhi yenu wamepokea mikopo ya zaidi ya milioni tisini tungependa utaratibu huo ni kawaida,” ameeleza Mwariko.
Mwakilishi wa Taaasisi ya kimataifa ya IITA anayeshughulikia elimu kwa vijana Bi. Veronica Kebwe amesema kazi yao ni kushirikiana na Halamashauri kupitia idara ya maendeleo ya jamaii kuwawezesha vijana kuziona fursa mpya za kilimo biashara kutokana na changamoto walizonazo kwa kuzingatia mawazo yao na kuwajengea uwezo na kuwasimamia ili kufikia lengo la kuondokana na tatizo la ajira.
Kwa uapande wake Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za jamii ya halmashauri ya mji Newala ambaye ni diwani wa Kata ya Namiyonga Mhe. Issa Mnayahe amesema kwa wale waliopata semina wanalo deni la kueneza elimu waliyopata kwa wananewala ili lengo Serikali kupitia Halmashauri la kuwawezesha wananchi litimie.
Aidha Mkuu wa idara ya kilimo wa Halmashauri ya mji Newala Bw. Calistus Komba amesema idara imejipanga kutengeneza vikundi vya wakulima vya uzalishaji mbegu bora na kuwasimamia ili kuleta tija ya kilimo jambo litakalotoa hamasa kwa vijanawengi kujikita kwenye shughuli za kilimo kutokana na fursa za kipato pamoja na mnyororo wa thamani kwenye kilimo.
Mmoja wa vijana walioshiriki mafunzo hayo Besti Alphonce Lihaya mkazi wa Luchingu Newala ambaye ni mfanya biashara ameishukuru Halmashauri kwa kuwa amenufaika sana na uwezeshaji uliofanyika hasa katika namna ya kujikita kwenye kilimo biashara nakubadilisha mawazo ya vijana kuhusu ajira na maisha halisi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa