Kamati ya mikopo pamoja na timu ya menejimenti ya halmashauri ya Mji Newala wamefanya ukaguzi wa shughuli za vikundi 39 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyoomba mikopo ikiwa ni hatua ya awali kabla ya utoaji wa mikopo.
Afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri hiyo Bi. Joyce Mramba amesema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya taratibu za kuhakikisha mikopo inayotolewa inawanufaisha walengwa waliokusudiwa na kusaidia miradi yenye tija ili walengwa waweze kufanya marejesha kwa wakati.
Aidha Mramba ameeleza kuwa mikopo hiyo hutolewa bila riba kwa vikundi vilivyosajiliwa rasmi na vinavyotekeleza miradi yao kama biashara ndogondogo, kilimo, ufugaji, ubanguaji wa korosho, na shughuli nyingine za uzalishaji kwa lengo la kuwainua kiuchumi.
Baadhi ya wanavikundi waliokaguliwa Bw. Ally Nalola na Bi. Sarah Mlaponi wameeleza kuwa ziara hiyo imewapa fursa ya kupata elimu pamoja na ushauri wa kitaalamu kuhusu uboreshaji wa miradi yao na kwamba wapo tayari kuzingatia masharti ya mikopo yatakayotolewa.
Halmashauri ya Mji Newala inatoa mikopo yake kwa kushirikia na benki ya NMB kwa mwaka wa fedha 2025/2026 imepanga kukopesha shilingi milioni 230 ambapo mpaka sasa imeshatoa mkopo wa shilingi milioni 59.2 katika awamu ya kwanza na sasa anatarajia kutoa mkopo wa awamu ya pili.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa