Viongozi wa serikali, siasa, dini na Taasisi zingine za kijamii wilayani Newala wametakiwa kuhakikisha wanasaidia kutoa elimu ya chanjo ya uviko 19 kwa wananchi wanaowaongoza ili kuwalinda na madhara ya ugonjwa wa korona yanayoweza kusababisha kifo.
Wito huo umetolewa leo Jumatatu Octoba 04, 2021 na mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Alhaj Rajabu Kundya wakati wa kikao cha uhamasishaji wa ndani ya jamii kuhusu chanjo hiyo kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Newala, kikiwahusisha madiwani, watu maarufu, watendaji wa kata na wadau wa maendeleo kwenye jamii wakiwemo watoa tiba asili.
Mhe. Kundya amesema kiongozi bora ni yule anayehakikisha afya za wananchi wake ni salama na kwakufanya hivyo utaweza kutekeleza mipango yako na kuinua maendeleo watu wako na ya taifa kwa ujumla hivyo kila mmoja ahamasishe jamii kupata chanjo kwani huo ndio mtaji salama kotokana na janga la uviko 19.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Newala Bi Shamim Mwarika ameameitaka jamii kutambua kuwa ugonjwa wa korona upo nani muhimu kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi mapya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Newala amewaonya watu wanaokwenda kutoa elimu kwa wananchi kuacha kuongea mitazamo yao binafsi badala yake waeleze hali hali kama miongozo ya wizara ya afya inavyoelekeza na sio kuwatisha watu na kuwaogopesha hata waliokuwa tayari kuchanja.
Aidha Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji Newala wakati anatoa hali ya ugonjwa ndani ya halmahauri hiyo amebainisha kuwa hali yasasa haidhirishi kwani hospitali ya Wilaya imepokea wagonjwa wengi kuanzia mwezi Julai kipindi ambacho wimbi la tatu la ungonjwa lilianza kuibuka, hivyo mpango wa serikali wakuwapatia chanjo wananchi unapaswa kuitikiwa kwa nguvu kubwa ili kuinusu jamii.
Mmoja wa wananchi waliodhuria kikao hicho Bw. Yasini Chiteha ameomba takwimu na taarifa za wagonjwa wa korona ziwekwe wazi kwa Mwanainchi ili kila jamii iweze kuelewa na ichuke maamuzi kutokana na hali halisi iliyopo hivi sasa.
Kwa hapa wialayani Newala kampeni ya uchanjaji harakishi kwa watu mwenye umri wa miaka kuanzia 18 linaendelea kwenye vituo vyote vya afya, zahanati na hospitali na litahitimishwa tarehe 14 octoba, 2021.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa