Jamii, wadau pamoja na Idara ya elimu Halmashauri ya Mji Newala, kwa pamoja wametakiwa kuchukua hatua za makusdi za kuongeza ufaulu ili kurejea katika nafasi yake.
Agizo hilo limetolewa leo Jumanne Machi 30, 2022 na kaimu Mkuu Wa wilaya ya Newala ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala ambae alikua mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Juma la elimu ngazi ya halmashauri yaliyofanyika viwanja vya sabasaba Newala mjini.
Kanali Sawala amesema taarifa ya elimu ineonyesha halmashauri hiyo ilikua ya kwanza kwa ufaulu ngazi ya mkoa kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2018 lakini matokea ya mwaka jana 2021 hayakua mazuri hivyo wazazi, wanafunzi,walimu na wadau wengine washikamane kwa mwaka 2022 kurudisha hali ya awali ya ufaulu.
Aidha Mkuu wa wilaya amesema kuwa pamoja na halmashauri kuwa na changamoto ya uhaba wa walimu, mbinu mbadala za ufundishaji zibuniwe ili kuongeza uelewa kwa wanafunzi hasa watahiniwa kwa lengo la kuendana na matarajio ya kuwa shuleni.
Maadhimisho ya Juma la Elimu mkoani mwaka huu 2022 yamebeka kaulimbiu isemayo "Tuwajibike Pamoja Kuleta Maendeleo Ya Elimu Mtwara."
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa