Wadau wa elimu halmashauri ya Mji Newala wameomba uwepo wa ushirikiano baina yao, wazazi, wataalam wa elimu pamoja na wanafunzi utakaosaidia kuinua kiwango cha elimu.
Wameyaeleza hayo katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ambapo wameitaka jamii kushiriki kwa vitendo katika kufundisha kwa njia ya malezi, kuchangia chakula cha wanafunzi, kuchangia mfuko wa elimu pamoja na kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi.
Kwa upande wake mwakilisha wa wenyeviti wa kamati za shule Bi. Mwanahamisi Songa amekiri kuwa wazazi wapo nyuma katika kusaidia ukuaji wa elimu “mimi naamini watataalam kazi yao wanafanya vizuri shida ipo kwetu sisi wazazi hatuoneshi ushirikiano watoto wanatupwa hovyo”.
Mwalimu Ibrahimu Adamu wa shule ya Msingi Makonga ameongeza kuwa wazazi wanashindwa kufuatilia mwenendo wa elimu ya watoto wao “ningeomba viongozi wale wazazi kule nyumbani tuwape semina kwamba mtoto akirudi shuleni basi yeye kazi yake ni nyumbani”.
Naye Mwalimu kiongozi wa kutoka shule ya msingi Makote, Mwl. Nunu Kupela ameomba ogezeko la walimu wa muda kupitia fedha za mfuko wa elimu ambapo ameeleza kuwa pamoja na mfuko huo kufanya vizuri katika miundombinu kwasasa iangalie suala la kuongeza walimu wa muda.
Aidha afisa mwakilishi wa jeshi la polisi wilayani Newala Derick Lekayo ameitaka jamii kuwapunguzia watoto muda wa kushiriki mambo ya kitamaduni hasa ngoma za unyango na mikesha ya sherehe.
“Kuna ngoma za kitamaduni tilizonazo katika wilaya yetu, ngoma hizo zina madhara makubwa sana kwenye maendeleo ya elimu, hizo ngoma ni nzuri ziendelezwe kwasababu ni utamaduni wa watu lakini ziwe na mda rafiki kwa watoto”
Hata hiyo Mwenyekiti wa shule ya msingi Nangwanda iliyopo kata ya Mcholi I Ndg. Abillah Mniha ameshauri, idara ya elimu ifanye mgawanyo wa walimu kwa uwiano wa wanafunzi katika shule ili kusaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa walimu.
Katika taarifa ya ulaji wa chakula shuleni imeonyesha asilimia 85 pekee ya wanafunzi wa shule za msingi ndio wanaopata chakula shuleni na upande wa sekondari shule zote zinatoa chakula lakini si wanafunzi wote wanaokula kutokana na wazazi wao kutochangia.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa