Wakulima wa Alizeti wameishukuru Halmashauri ya Mji Newala kwa jitaihada zake za kuwasaidia kupata elimu na ushauri wa kukuza kilimo cha zao hilo mbadala katika kukabiliana na changamoto ya kiuchumi kwenye kilimo.
Bwana Hamadi Kadembe ambaye ni mkulima wa zao hilo amesema haikuwa rahisi kwake kuanza kulima zao hilo, lakini anaishukuru idara ya kilimo Halmashauri ya Mji Newala kupitia wataalam wake wamewajengea uwezo na kuwapa mafunzo katika hatua za kufikia uzalishaji wenye tija.
Kadembe amesema huu ni mwaka wake wa tatu tangu ameanza kulima alizeti na ameweza kukabiliana na changamoto za kimaisha kwa kuwa kilimo hicho kinampatia kipato tofauti na mtazamo wa wengi wanaodhani kulima zao hilo ni kupoteza muda kwa kuwa halina faida.
“Nimekua nikifuata kanuni na maelekezo ya maafisa kilimo wa Halmashauri ya Mji, huwa wanakuja kunitembelea na kuona tunalimaje, kasha wananishauri nifanye nini, kwa kweli wananitia moyo sana, mwanzoni nilikua nifeli kwenye korosho ndio basi lakini sasa nauza mafuta ya alizeti, napata kipato naendesha maisha ya familia yangu vizuri.” Alieleza Mkulima huyo.
Kwa upande wake Bi. Mariam Machemba mkulima wa mazao mchanganyiko anasema analima zao la Alizeti kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na biashara kutokana na maarifa aliyopata kutoka kwa wataalam wa kilimo na kwasasa anazalisha mafuta kiasi cha kuwauzia wafanya biashara wengine.
Aidha Bi. Machemba amewataka wanawake kubadili mitazamo yao na kuchangamkia kilimo hicho kwa kuwa kinamuwezesha kulipia mahitaji ya watoto shuleni, kumpatia mahitaji ya nyumbani pamoja na mahitaji binafsi.
Hata hivyo ameleeza kuwa changamoto za kulima Alizeti kulinganisha na mazao mengine na jambo kubwa ni kujua muda sahihi wa kupanda mbegu na hiyo inatokana na upya wa zao lenyewe. “wakati mwingine nashindwa kupata mazao yakutosha kutona na kuwahi au kuchelewa kupanda sehemu hiyo bado sijajua vizuri japo maafisa kilimo wananitembelea mara kwa mara shambani kwangu”.
Bwana Calistus Komba amesema kilimo cha Alizeti ni mpango wa Halmashauri kuhamasisha wananchi kulima mazao mbadala na kitu cha kufurahisha kuona mwitikio unaridhisha kila mwaka uzalishaji unaongezeka na wakulima wanaongezeka japo lengo kusudiwa bado halijafikiwa.
Aidha amesema halmashauri pamoja na kuhamasisha kupitia maafisa ugani lakini pia inawezesha katika ununuzi wa mbegu bora, kutambua maeneo yanayofaa kwa kilimo hizo pamoja na kununua mashine za kukamulia ambazo zinakabidhiwa kwenye vikundi vya wakulima wenyewe wazisimamie.
Halmashauri ya Mji Newala ni moja ya halmashauri ambazo zimekuwa kwenye jitihada kubwa ya kuinua uchumi kupitia kilimo cha mazao mbadala nje ya zao mama la Korosho kwa kuwekeza katika mazao ya Alizeti, Mpunga, Ufuta na Muhongo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa